@bongo.trendingtz: Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amesema ili kufanikisha Mkakati wa Watoto kujua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) ni lazima kuwe na ushirikiano na ufuatiliaji wa Mzazi na Mwalimu. Mtaka amesema hayo wakati wa kufungua Kikao cha Viongozi wa Mkoa wa Njombe na Mradi ‘Kijiji Changu’ unaofadhiliwa na Uwezo Tanzania unaolenga kumalizia Changamoto ya Watoto kutokujua Kusoma, Kuhesabu na Kusoma. Ametaja mfano wa Mtoto ambaye alifanyiwa Sherehe na Wazazi wake kufika Darasa la Tatu hajui kusoma, kuandika na kuhesabu. #bongotrendingtz #tanzaniantiktok🇹🇿 #kenyantiktok #ugandatiktok🇺🇬 #reatorsearchinsights