@bongofive: Suge Knight, aliyekuwa akiendesha gari ambalo Tupac Shakur alikuwa ndani yake usiku wa shambulio la mwaka 1996, amesema hataki kwenda mahakamani kutoa ushahidi katika kesi ya mauaji ya Tupac. Suge Knight amesema kesi hiyo haihusiani naye na ameomba aachwe nje ya mchakato huo. Wakati huo huo, Duane “Keefe D” Davis, ambaye ndiye mtu pekee aliyeshtakiwa rasmi kwa mauaji ya Tupac, tayari ameanza kusikilizwa mahakamani Las Vegas. Kwa sasa kesi iko kwenye hatua ya uchaguzi wa majaji, huku Keefe D akiendelea kukana shtaka la mauaji. 🎤…… @cathed__