@kusagatv: SEFU MUSA ADAIWA KUAWA NA ASKARI BAADA YA KUTUHUMIWA KUWA MJANGILI NGORONGORO Kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Sefu Musa amefariki dunia baada ya kudaiwa kuuawa na askari watatu katika eneo la Ngorongoro mkoani Arusha, baada ya yeye na wenzake kutuhumiwa kuwa ni majangili. Sefu alikuwa pamoja na Salim Hamisi maarufu Pachaa na Abdallah Nuru, wakitokea Arusha mjini kuelekea Babati mkoani Manyara kwa ajili ya kumzika mwenzao ambaye walikuwa wakifanya naye kazi ya kutengeneza magari maeneo ya Desemba jijini Arusha. Watatu hao walikuwa wamepanda pikipiki moja na walipofika Makuyuni walipotea njia na kuelekea Karatu badala ya Babati. Waliendelea hadi Karatu mjini na kufika katika lango la kwanza la Ngorongoro lililokuwa likilindwa na askari watatu. Baada ya kufika lango kuu la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro walibaini kuwa wamepotea njia na wakaamua kurejea. Inadaiwa walipofika katika lango la kwanza walikamatwa na askari hao na kutuhumiwa kuwa ni majangili, licha ya kueleza kuwa walikuwa wamepotea na walikuwa wakielekea Babati kwa ajili ya mazishi. Kwa mujibu wa maelezo ya Abdallah Nuru, ambaye ndiye aliyenusurika, vijana hao waliamriwa kuvua nguo na kujigaragaza kwenye majani yaliyokuwa yakiwasha huku wakimwagiwa maji na askari hao, kabla ya kudaiwa kupigwa. Katika tukio hilo, Sefu Musa alidaiwa kuzidiwa nguvu na kupoteza fahamu huku Salim Hamisi naye akizimia. Abdallah anadaiwa kupata majeraha mbalimbali lakini aliendelea kuwa na nguvu na kuwasaidia wenzake. Baada ya hali kuwa mbaya, inadaiwa waliambiwa wavae nguo na kuondoka eneo hilo. Abdallah alitafuta bajaji na kuwapeleka wenzake katika Hospitali ya Lutheran Karatu. Walipofika hospitalini, Sefu alikutwa amefariki dunia huku Salim akiwa katika hali mbaya na kupewa huduma ya oksijeni iliyomsaidia kurejea kwenye fahamu. Anaendelea kupatiwa matibabu. Abdallah Nuru ndiye aliyenusurika na kufanikiwa kuwasaidia wenzake hadi hospitalini licha ya yeye mwenyewe kupata majeraha. Mwili wa Sefu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti. Tumempigia simu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kupata ufafanuzi kuhusu taarifa hiyo, lakini simu yake iliita bila kupokelewa. Taarifa zaidi zinaendelea kufuatiliwa ili kupata undani wa mazingira ya kifo cha Sefu Musa.
MWANDISHI WA WANANCHI
Region: TZ
Wednesday 12 August 2026 17:23:18 GMT
Music
Download
Comments
alhamhappy :
Nimejua kulia mimi jamani😭MUNGU naomba tusaidie🙌🏾
2026-08-12 18:00:41
59
honey :
amna siku nimeingia ticktock sijakutana na tukio ARUSHA🙌🙌🙌
2026-08-12 18:29:46
54
farihina khalidi :
lakn naisi so hii tanzania mbn tunanyanyasika kwann
2026-08-12 17:50:16
79
Sweet_john :
Mungu awalaani ao maaskari
2026-08-12 17:41:49
94
winnie3900 :
Mungu ikikupendeza hao askari nakuomba yesu wangu😭😭😭
2026-08-12 17:55:59
163
DADA MKUBWA💞💞🇹🇿 :
eeemungu sikiya kilio cha watu wako😭😭
2026-08-12 17:34:57
151
Abel Laizer :
afu mseme tuna urafiki na mapolisi sisi na polisi ni maadui na hii vita itafika mbali
2026-08-12 17:46:12
136
____Gifted____.🦋🌸 :
YANI MPAKA MWANAUME ANAMWAGA MACHOZI UJUE KAUMIA SANA😭
2026-08-12 18:56:00
43
Ester :
pole sn 😭😭😭😭😭
2026-08-12 20:14:16
0
Maasai herbs point :
hamkutii amri
2026-08-12 17:38:26
10
bi ruu og :
sheriaitate
2026-08-12 20:22:47
0
Mom5 :
Am speechless
2026-08-12 20:31:46
0
Mariah Mgimwa :
policeman 👮♂️
2026-08-12 19:23:28
0
Ridah🦋 :
Kuna maskali wengne ni waonevu kiukweli inaumiza sana😭
2026-08-12 18:09:17
25
abushehe :
duu noma sana
2026-08-12 19:57:28
0
silah Looh :
mmmmmm? mmh
2026-08-12 20:26:30
0
muddy6shots :
Sheria za hifadh zipo wazi kiubinadam hao jamaa wamekosea ila ukijua mtiti wa jangili hutalaumu...kila kifo kina sababu Mungu ndio anajua kila jambo
2026-08-12 18:17:40
5
angle❤️ :
ila damu ya mtu aiendi bure 😳😳😳
2026-08-12 17:55:50
32
johnson :
mimi na police ni mbalimbali
2026-08-12 18:04:49
15
𝑽𝒐𝒏❀🫧 :
Ameongea kwa uchungu"ukipata na nafasi ya kumsaidia mtu msidie tu"😭
2026-08-12 19:08:12
16
zamda :
jamani mapolisi hebu jaribuni kuwa nautu jamani hii Dunia tunapita Kila nafsi itaonja umauti hakuna ataebaki hapa duniani milele😢😢
2026-08-12 18:16:51
19
kadari :
hiii ndio nchi mnyama anathamani kuliko binadamu ogopa sana yani duuh poleni sana ila mungu yupo
2026-08-12 18:53:20
14
Bint Canizio :
Machozi yamenitoka, ila hao Askari wasisahau kuwa baada ya kazi kuna maisha kesho yao hawaijui kwahyo wasikose utu namna hyo
2026-08-12 19:15:10
14
Hoc :
😭wanawinda nini bila silaha uonevu umezidi askar acheni makasiriko hii ni fedhea kabisa🫤
2026-08-12 19:46:02
11
To see more videos from user @kusagatv, please go to the Tikwm
homepage.