@wepesitv: Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 45 amekamatwa na wananchi katika Mtaa wa Mbugani, Kata ya Magugu, Wilaya ya Babati mkoani Manyara, akidaiwa kuingia usiku katika boma la jirani yake na kuchimba dawa, huku akiwa na kisu na nyoka. Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mbugani, Jonathan Daudi Wamo, amesema alipata taarifa kutoka kwa vijana kwamba mwanamke huyo amekamatwa, na alipofika eneo la tukio alimhoji na kumtaka aoneshe alikoficha dawa hizo. Amesema mwanamke huyo alifukua dawa zilizokuwa zimefungwa katika kitambaa cheusi na kudai kuwa alielekezwa na mganga ambaye aliwasiliana naye kwa njia ya simu, akiamini kuwa jirani yake ndiye aliyesababisha matatizo ya kiafya aliyokuwa akiyapata. Kwa upande wake, mwanamke huyo amekiri kufika katika eneo hilo usiku na kusema hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kushawishika kufanya kitendo hicho, huku akiwaomba wananchi na serikali wamsamehe na kuahidi kutorudia tena. Mwenyekiti huyo amesema viongozi wamechukua hatua za awali kwa kulinda eneo na kumsubiri mwenye nyumba pamoja na viongozi wengine ili hatua zaidi zichukuliwe.
WEPESI TV
Region: TZ
Thursday 13 August 2026 04:15:24 GMT
Music
Download
Comments
Musa Mawele :
video
2026-08-13 08:21:50
1
mack :
aibu hii ya nini
2026-08-13 14:21:54
0
🤍Lillycruiser ✨ :
Kanisani kufanyaje jmn 😳 bora umwamini mlevi
2026-08-14 18:25:39
0
Minah :
dah sasa mbn mwenye mama ni aibu tupu jamn mung atuepushie mama vituk n ving mnoo
2026-08-13 19:45:51
0
Farid Rashid :
😅
2026-08-15 20:15:01
0
namchik💫 :
🙏🙏🙏
2026-08-13 11:10:17
0
To see more videos from user @wepesitv, please go to the Tikwm
homepage.