@dunialeo_: Mjumbe wa Tanzania Hajj Federation (TAHAFE), Mohammed Nassoro, amesema taasisi 19 zimesajiliwa na kupitishwa rasmi kwa ajili ya kupeleka mahujaji katika ibada ya Hijja kwa mwaka 2026/27. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Nassoro amesema taasisi hizo zimepitishwa baada ya kukidhi taratibu zinazohitajika, ikiwemo usajili na utaratibu wa gharama za huduma za Hijja. Ametaja baadhi ya taasisi hizo kuwa ni Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Basigadil, M23, Kidudo Tours, Ahluka na Advert, huku akisema jumla ya taasisi zilizoruhusiwa ni 19. Nassoro amewashauri mahujaji wanaotarajia kwenda Hijja kutumia taasisi hizo zilizopitishwa na mamlaka, badala ya kufanya taratibu kupitia taasisi ambazo hazijasajiliwa au kupitishwa.#dunialeoUPDATES

DuniaLeo
DuniaLeo
Open In TikTok:
Region: TZ
Friday 14 August 2026 16:57:07 GMT
1478
21
3
7

Music

Download

Comments

jmk_2024
🌴 :
Nahisi hizi ni taasisi za Tanzania bara
2026-08-20 18:48:36
0
bbyjally41jr
jly,🏔️❄️ :
mbona bakwata walisema ni wao tu!!!
2026-08-20 19:48:58
0
salamiseifalriyam
salamiseifAl-riyami :
iskama hawamo
2026-08-20 16:10:24
0
To see more videos from user @dunialeo_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About