@wananchiitv: Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP Centre), David Kafulila, amefanya uchambuzi wa kina wa kifalsafa na kiuchumi kuhusu maana halisi ya maendeleo endelevu, akisisitiza kuwa uwekezaji mkubwa zaidi ambao taifa lolote linapaswa kuufanya ni katika ubora wa rasilimali watu. Kafulila amesema hayo akihutubia mamia ya wakufunzi, na wanafunzi katika Mhadhara wa Umma uliofanyika Agosti 14, 2026, katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD) kilichopo jijini Arusha. Kafulila alirejea historia ya harakati za ukombozi wa nchi na kuweka wazi kuwa misingi ya maendeleo yanayomlenga mwananchi (people-centered development) iliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, tangu mwanzo kabisa mwa safari ya kudai uhuru. Alinukuu hotuba ya kihistoria ya Mwalimu Nyerere aliyoitoa kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa (UN) mwaka 1958, ambapo alibainisha kuwa msingi wa Watanganyika kudai mamlaka yao haukuwa chuki au ubaguzi wa rangi dhidi ya wakoloni wa Kiingereza, bali ni kutokana na ukweli kwamba utawala huo ulishindwa kutokomeza maadui wakuu watatu wa maendeleo ambao ni ujinga, maradhi, na umaskini. Kafulila aliongeza kuwa mtazamo huo wa Mwalimu Nyerere ulikuwa mchango wa kubadilisha muelekeo wa dunia kutoka Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) hadi kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya sasa (SDGs). Alieleza nchi inapojenga miradi mikubwa kama barabara, stendi, miundo mbinu ya huduma za kijamii na madaraja kwa njia ya ubia(PPP), msingi wa uamuzi huo ni maendeleo ya watu kwani vitu hivi vinaongeza uwezo wa watu kuzalisha katika shughuli zao za kila siku. FALSAFA YA NYERERE INAISHIAJE KWENYE PPP?……. Tuambie kwenye maoni hapo chini

Wananchi Tv
Wananchi Tv
Open In TikTok:
Region: TZ
Saturday 15 August 2026 07:39:03 GMT
395
20
0
0

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @wananchiitv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About