@veriafya: Akizungumza na Veriafya, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi, Godfrey Chale wa Dkt. Chale Polyclinic iliyopo Mbezi kwa Msuguri anabainisha kuwa takriban 50% ya matatizo ya uzazi kwa mwanamke husababishwa na mvurugiko wa homoni kwenye vichocheo vinavyodhibiti mzunguko wa hedhi na upevushaji wa mayai, wakati 50% nyingine inatokana na changamoto za kiumbe katika viungo vya uzazi kama vile uvimbe na maambukizi yanayoweza kuharibu kuta za kizazi au kuziba mirija ya uzazi na kuzuia mbegu na yai kukutana au kusababisha mimba kutungia nje ya mji wa uzazi Ufafanuzi kamili wa mazungumzo haya unaweza kuupata hapa https://youtu.be/A5Qa6RUHWNw?si=0fOVoM4VlOmmhz3R