@mt..rita.wa.casia: ๐น ROZARI TAKATIFU ๐น ๐ TUSALI KWA IMANI KUU ๐ ๐ฟ JUMATANO & JUMAPILI โจ MATENDO YA UTUKUFU โจ ๐ NIA YETU KUU ๐ Mama Yetu Bikira Maria, tunakushukuru kwa baraka na neema zako. Leo tunakukabidhi Rozari hii pamoja na mahitaji yetu yote. ๐น Waangalie wagonjwa na wadhofu, ๐น waangalie wakosefu, ๐น ndoa na familia zetu, ๐น kazi, biashara na utume wetu, ๐น watoto na wazazi wetu, ๐น Kanisa na Wakristo wenzetu, ๐น pamoja na Taifa letu. Mama Maria, tunakuomba utuombee na utupeleke kwa Mwanao Yesu. Amina. ๐ โโโโโโโโโโโโโโ ๐ฟ MATENDO YA UTUKUFU 1๏ธโฃ TENDO LA KWANZA โ๏ธ Yesu anafufuka. ๐ Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu. 2๏ธโฃ TENDO LA PILI โ๏ธ Yesu anapaa mbinguni. ๐ Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni. 3๏ธโฃ TENDO LA TATU ๐ฅ Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. ๐ Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu. 4๏ธโฃ TENDO LA NNE ๐น Bikira Maria anapalizwa mbinguni. ๐ Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri. 5๏ธโฃ TENDO LA TANO ๐ Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni. ๐ Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema. โโโโโโโโโโโโโโ ๐ฟ KATIKA KILA TENDO: ๐ Baba Yetu ๐น Salamu Maria ร 10 โ๏ธ Atukuzwe Baba โค๏ธ Tuwasifu milele, Yesu, Maria na Yosefu. Ee Yesu mwema, utusamehe dhambi zetu, utukinge na moto wa milele, uongoze roho zote mbinguni, hasa zile zinazohitaji zaidi huruma yako. โโโโโโโโโโโโโโ ๐น SALAMU MALKIA ๐น Salamu, Malkia, Mama mwenye huruma; uzima, tulizo na matumaini yetu, salamu. Tunakulilia katika bonde hili la machozi. Ee mwombezi wetu, utuangalie kwa macho yako yenye huruma, na mwisho wa ugeni huu utuoneshe Yesu, mzao mbarikiwa wa tumbo lako. ๐ Mama Maria, Malkia wa Rozari Takatifu, utuombee. โค๏ธ Yesu, Maria na Yosefu, tunawapenda. Tuokoe roho zetu. โ๏ธ Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina. #RozariTakatifu #MatendoYaUtukufu #MamaMaria #relatable #tiktoktanzania๐น๐ฟ
Mt. Rita wa casia
Region: TZ
Sunday 16 August 2026 16:05:18 GMT
Music
Download
Comments
James King'oo :
pray for us blessed mary amen
2026-08-20 05:15:30
0
Suzy Suzy from mbale city :
holy Mary Mather of God pray for us ๐๐
2026-08-19 12:35:29
0
@MaryCharles :
mtakatifu rita wa kashia utuombee๐๐๐
2026-08-18 06:33:49
15
๐ฅ๐ Elizabeth๐ซ Lizzy ๐ฅ๐๐ :
amen ubarikiwe kpnz ktkt bwana
2026-08-17 18:18:18
9
nuuh :
ewe mama Maria utuombee ss wakosefu Amina
2026-08-18 06:51:21
8
Estherrodrick :
kwani icho kitabu shingapi na kinaitwaje please nakihitaji
2026-08-18 08:41:11
5
user537956327048 :
Eeee Bikira maria mama wa mkomboz utuombeee SS wakosefu Ameni
2026-08-18 04:51:02
4
Rose Abdala :
Mtakatifu rita wakashia utuombee
2026-08-18 07:56:39
1
Valentina Charles :
iki kitabu kinaitwaje
2026-08-17 11:05:04
1
Thee Roberto โจโจ :
Any pdf format of the book?
2026-08-18 15:49:16
1
kevoo :
Ee bikira Maria nakuomba uniombee Amina ๐๐๐
2026-08-18 12:52:23
2
Naomi mkami๐ :
naomba niunge namimi
2026-08-17 15:03:28
2
alantz :
natafta hiki kitabu
2026-08-16 17:16:13
1
Melania Joseph :
mama maria utuombed
2026-08-18 06:44:43
1
Baba BON/BLAS :
nashida na Iko kitabu
2026-08-18 19:03:56
0
felly Paul๐ :
Mt Rita wa kashia utuombeee๐
2026-08-17 15:50:15
1
Irene mwende :
nakimbilia kwako mom๐๐๐๐
2026-08-17 17:34:05
1
user7939021618761 :
tumsifu yesu kristo namsbukulu mungu kwa kuzaliwa mwezi wa rozari
2026-08-19 07:43:56
1
Veronica :
Amina
2026-08-17 16:18:07
1
user2003331533441 :
Mimi nasali Holy Rosary siku ya Alhamisi bila kukosa.
2026-08-18 11:40:18
1
Amina Mgala :
nahitaji kitabu
2026-08-20 08:37:44
1
mourine tz :
mt Lita utuombee
2026-08-20 18:06:33
0
user7373598145026 :
Amina mama MARIA utuombee
2026-08-20 17:32:44
0
Clรฉmentine amuli :
maman wauruma utuombeee
2026-08-20 17:58:43
0
Vero :
Amen ๐๐๐๐๐๐
2026-08-20 19:19:33
0
To see more videos from user @mt..rita.wa.casia, please go to the Tikwm
homepage.