@power_media08: KAY MZIWANDA BAADA YA KUWANYOOSHA TAKATAKA WA JAY RYTTY SASA AWAGEUKIA TAKATAKA WA MO DEWJI 'WAZEE MTUKOME' Nafikiri kwa sasa wale mashabiki na wanachama wa Simba SC yenyewe na sio Jay-Rutty SC wala Mo Dewji SC na Mangungu SC watakua wanakubaliana kwa kila neno na Kay Mziwanda ambae ameamua kukemea makundi yanayoendelea kumea ndani ya timu yao. Kay Mziwanda acheki na yoyote na ameamua kujivisha mabomu na kubeba silaha nzito na nyepesi na kuingia vitani kuwasambaratisha wale mashabiki na wanachama ambao yeye anawaita ni 'machawa' na ni 'takataka' 'mashabiki njaa' wanaotaka kuipasua Simba SC vipande vipande. Bila kuvaa darubini ya kuona mbali, kwa macho tu ya nyama kwa sasa ukiangalia Simba SC unaona kuna makundi na matabaka kinzani. Kuna kundi linalomtetea Mzabuni wa Jezi Jay-Rutty na wapo wafia Mo Dewji ambao wanamuombea mabaya Mzabuni wa jezi akwame kwenye mauzo ya jezi, Irizar likiaribu wao wana furahia na wanaposti mitandaoni na kushindwa kusajiliwa Feisal wamefanya mpaka 'House Party' kusheherekea. Na kuna kikundi sio kikubwa wala sio kidogo cha Chair man hili ni kundi linaloungwa mkono na 'takataka' na 'chawa' wengi wanaotoka upande wa Mzabuni wa jezi japo wapo na 'Wafia Mo Dewji' wachache wanaoingia na kutoka ambao wao wanapush agenda ya kutaka katiba iliyofanyiwa marekebisho na kuruhusiwa na vyombo halali vya Serikali ianze kutumika. Na hawa ni wataalamu wanajua wanachokifanya na wanajua nini kitakwenda kutoa endapo Katiba mpya ikianza kutumika, wapo nondo wameshamezeshwa maneno ya kua kama Katiba iliyoboreshwa ikianza kutumika itatamka wazi wawekezaji wataanzia watatu na sio kama ilivyo sasa tajiri ni mmoja tu. Na kama akikasirika anasema lolote analojisikia na hakuna mlango wa kutokea, na kwao wanaona Yanga SC ni kama wamefanikiwa kwenye mfumo wao mana wao wanahubiri wazi wazi wawekezaji kwao wataanzia watatu sasa kwanini Simba SC wao wabakishwe kwa mtu mmoja tu? Na wanaotaka Katiba mpya ianze kazi mara moja wanaamini ikianza kazi hakutakua na bodi ya udhamini na uendeshaji ambayo wao kwa sasa wanaiona ni bodi inayorimotiwa na mtu mmoja ambaye ni Rais wao wa Heshima na kwa kiasi kikubwa wanaamini pia ni sehemu ya kumkwamisha mzabuni wa Jezi.

Power media
Power media
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 18 August 2026 03:32:03 GMT
43074
1571
129
31

Music

Download

Comments

user6763228477308
Marco Naftal Siuhi :
K Mziwanda wewe ni mwanamke wa Nguvu sana umenyooka mimi nakupenda sana kwa fact zako wewe ni mkweli naungana na wewe
2026-08-18 08:16:06
24
zaituni.mahiga
🥰💐baby zuu💐💐🥰🥰 :
uko fact
2026-08-18 20:43:48
0
kassimndomba63
NICE BOY :
dada ukofact
2026-08-18 19:43:48
0
abdul.tz19
ABDULLA TZ✈. :
exactly 💯.
2026-08-18 09:28:48
0
mtega044
Hussein :
Sema hii video ungepost tiktok ingetrend sana😁😁
2026-08-18 12:23:15
4
keneth2550
April 24 🇹🇿🇵🇹 :
Yan kumbe Mo alikua anaikopa Simba na sio kutoa pesa kama mzamini
2026-08-18 08:43:03
5
ukwelimchungu2
MR.X :
Simba irudi kwa Wanachama kwanza kisha Mchakato wa Udhamini ufanyike..Matatizo yote ya Simba ni Mo Dewji
2026-08-18 10:24:07
2
user4723026963812
user4723026963812 :
twendeni kwa jakaya mlisho kikwete tumwambie kilio chetu
2026-08-18 04:23:46
1
loyce.mafuru
Loyce Mafuru :
watuachie Simba yetu atujawaita makelele tu Kila siku si waende wanakotak kwenda kwan Kuna mtu kawazuia au Kuna mtu amewambia lazima washabikie Simba waende tumewachoka
2026-08-18 07:55:51
4
tumainisomela
tumain :
kweli kbs
2026-08-18 08:44:25
2
user2361198763754
yotham jb :
Eee wachane ukweli,alafu hao wazee ndio wana wanaalibu timu yani
2026-08-18 09:26:53
1
japhetgoliama4
japhetgoliama4 :
Mnakumbuka pale jangwani mlifanya nni kwaiyo mtakologana sana
2026-08-18 06:38:35
1
adelafrancis
adelafrancis :
Wambie kabisa
2026-08-19 13:11:45
0
mohamedmbinga375
mohamedi.bakari.mbinga :
K MZIWANDA UNAONGEA POINT MUHIMU SANA FLUENCERS WENGI WANANJAA SANA
2026-08-18 08:03:03
1
sanganyamsanu
Sang'anya Msanu :
Kwani timu yenyewe inasemaje?
2026-08-18 16:13:13
1
allyramadhani6
allyramadhani6 :
kuna muda huyu dada ni kama namwelewa ,Kwa usemaji wake ,ila washabiki wa Simba ifike mahali ,tutimizo kauli ya Simba nguvu moja .mengine ya nn?
2026-08-18 06:32:58
1
user4103817168510
Sara jonas :
kabisa yan wana tuchosha mungu qtusaidie leo na pamba atuvushe kwa ili
2026-08-19 11:53:08
0
ally_nyota_graphics
Ally_Nyota Decorations ✨ :
Mangungu atuachie timu yetu
2026-08-18 10:38:58
1
ommywhitelukona
Ommy White Lukona :
nakuelewa sana K mziwanda mitano tena Mungu akutunze Dada yangu
2026-08-19 09:13:09
0
user4805140057150
Hayman luckman :
kweli kbsaaa watuwaheshimianee
2026-08-19 06:20:07
0
user5016356235732
user5016356235732 :
waambie kabisa sisi huku mitaani ndio tumechoka haswaaa tupumzisheni tuwe nguvu moja ya kweli sio ya kinafiki
2026-08-19 15:53:11
0
fatuma.lukombe
Fatuma Lukombe :
NI SIMBA NGUVU MOJA
2026-08-19 16:38:10
0
samsonedward714
@samsonedward714 :
kwani simba siku hizi hamna vikao mpaka watu wanalumbana mitandaon mbona yanga hatuyasikui?
2026-08-19 08:55:45
0
mtega044
Hussein :
2026-08-18 12:23:24
1
To see more videos from user @power_media08, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About