@cawabemedia_: Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando, ametoa agizo kwa mabasi yote yanayofanya safari kutoka Dar es Salaam kuanzia katika Stendi ya Mabasi Magufuli, akisisitiza kuwa mabasi yatakayokiuka utaratibu huo hayataruhusiwa kuendelea na safari. Msando ametoa kauli hiyo Agosti 17, 2026, baada ya kutembelea na kukagua hali ya vituo visivyo rasmi vya mabasi katika maeneo ya Shekilango (Urafiki) na Manzese. Amesema hatua hiyo ni sehemu ya maandalizi ya utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam linalotaka mabasi yote yanayofanya safari kutoka jijini humo kupakia na kushusha abiria katika Stendi ya Mabasi Magufuli. Kwa mujibu wa Msando, Serikali itaweka vituo maalumu vya ukaguzi (Check Point) katika maeneo mbalimbali, ikiwemo Barabara ya Morogoro, Sam Nujoma kuelekea Mwenge pamoja na maeneo mengine. Amesema vituo hivyo vitatumika kubaini mabasi yanayokiuka utaratibu, kuyazuia na kuchukua hatua dhidi ya waendeshaji watakaokaidi agizo hilo. Zoezi la utekelezaji wa agizo hilo linatarajiwa kuanza rasmi kesho, Agosti 18, 2026, huku mamlaka zikisisitiza kuwa mabasi yote yanapaswa kuzingatia utaratibu mpya. Hatua hiyo inalenga kuondoa vituo visivyo rasmi vya mabasi, kurahisisha usimamizi wa usafirishaji na kuhakikisha shughuli za kupakia na kushusha abiria Dar es Salaam zinafanyika kwa utaratibu unaotakiwa.
cawabemedia
Region: TZ
Tuesday 18 August 2026 07:02:14 GMT
Music
Download
Comments
wawa :
Hii ishu ni ngumu na mnawachokoza watu ambao wametulia
2026-08-18 08:17:51
7
Amani :
kwakweli tuwe na uniformity mabasi yote yawe stend ya magufuliii..
2026-08-18 10:10:56
4
Badru Salum :
Sasa mliwapa vitality vya nini vya kujenga terminal zao watu wameshanunua wamewekeza halafu mnazingua
2026-08-18 08:32:00
5
Driver001✅️ :
KUIBIWA KUMERUDI MAANA MAGUFULI KUNA WEZI SANA NA KINGINE MTU ATOKE CHANIKA MPAKA MAGUFULI MNAANGALIA NA WATUMIAJI AU MNATOA TAMKO BILA KUHAKIKI VIONGOZI MUWE MNAFWATILIA KABLA YA KUTOA MAAMUZI 🤝
2026-08-18 10:54:05
2
james :
Mkuu amri MOJA mabasi yote magufuli tumeona malori yote yameondoka pale uasibu kulasini Temeke.Mji unatakiwa iwe na mpangilio.
2026-08-18 11:56:28
3
rogous :
jamn naomba esther luxury wapen kibali wabaki shekilango
2026-08-18 08:06:27
4
MASSAWE :
NASISI ABIRIA MTUSIKILIZE TUNATAKA NINI MAANA WAO WAMEWEKA KUTOKANA NA SISI ABIRIA .
2026-08-18 09:40:57
1
akibarikabenzakab :
kabla yamamuzi mlitakiwa muaite wamiliki alafu mamuzi hayo yapte
2026-08-18 08:37:44
1
shacao :
LATRA wamenenepa hata kucheka ni tabu. hii nchi🤣🤣🤣🤣🤣
2026-08-18 09:25:03
2
mc471axb :
Swali ni kwamba Magufuli stand patatosha?
2026-08-18 09:26:29
2
Said kifaranga :
Huu ndio usumbufu sasa Mutawezaje kukagua magari Siku ya safari
2026-08-18 09:25:58
1
Victoria GL :
tutakuwa tunapandia buses kituo Cha kibaha na kushukia kibaha, ebo
2026-08-18 09:37:36
1
DACY :
ABOOD ANA MABASI 200 a zaidi SHABIBY BUS 150 BM 100 na Zaid na hiyo stendi inauwezo ya kukaa mabasi 200 tu
2026-08-18 13:18:01
1
Godson Mwangama :
Acheni kulazimisha vitu visivyowezekana,yaani mtu atoke mjini aende stand ya magufuli huko kibamba haiingii kichwani
2026-08-18 08:42:57
0
allymushi36 :
sijui ni nan atakae penda serekali hii kwa mambo haya ya ajabu namna hii ,watu wameshaingia gharama kubwa alafu mnawabadilikia hii sio sawa
2026-08-18 10:23:47
1
wawa :
Hivi nyie hua mnapigia hesabu ya gharama anayoipata abiria na usumbufu mpaka aende mbezi
2026-08-18 08:17:21
4
wawa :
Hii vita mnayoitaka hamtaiweza
2026-08-18 08:18:12
1
wawa :
Ktk hili mtatuua kwakweli
2026-08-18 08:19:19
1
njau :
ukisitisha safari anaumia abiria na sio wamiliki wa mabasi. lakini pia inaumiza abiria kutokea ndanindani kuja kwa magufuli stand so mtufikirie na sisi abiria.
2026-08-18 08:23:58
0
DarasaLetu :
Amri ambayo haina uwezeshi ni ngumu kutekelezeka.
2026-08-19 07:02:29
0
Yasinta John :
hii nnchi ngumu
2026-08-19 08:22:36
0
Isaack Bakaza :
Mbona tayari baadhi ya kampuni zimeishatii amri hiyo mfano alsaed
2026-08-18 20:48:25
0
Jamal Ismailly :
bos unataka kuwachokoza wawekezaji wa mabas kaka watakushindwa
2026-08-18 07:57:50
0
To see more videos from user @cawabemedia_, please go to the Tikwm
homepage.