@chawamata_tv: VIDEO: Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) kimetishia kuagiza malori kupaki nchi nzima iwapo agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, la kuyazuia malori kuegesha barabarani litaendelea kutekelezwa bila kuwepo maeneo mbadala ya maegesho. Akizungumza Agosti 18, Mwenyekiti wa TATOA, Elias Lukumay, amesema chama hicho hakipingi hatua za Serikali katika kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam, lakini kinataka mamlaka zitafute suluhisho la kudumu kwa kuwaondolea wamiliki wa malori mzigo wa kutafuta maeneo ya kuegesha magari yao. Lukumay amesema malori ni sehemu muhimu ya uchumi wa taifa, hasa katika kusafirisha mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda mikoa mbalimbali na nchi jirani, hivyo kuzuia malori kufanya kazi bila kuwepo kwa miundombinu ya kutosha kunaweza kuathiri mnyororo mzima wa usafirishaji. Amesema changamoto kubwa inayowakabili wasafirishaji ni upungufu wa miundombinu, akieleza kuwa lori linaweza kutumia kati ya saa nane hadi 10 kutoka Bandari ya Dar es Salaam hadi Kona ya Ubungo kutokana na msongamano wa magari. Mwenyekiti huyo amesema TATOA imekuwa ikishirikiana na Serikali katika kutatua changamoto za sekta ya usafirishaji, lakini imesikitishwa na hatua za kukamata malori, kuwavamia madereva na kung’oa namba za usajili, akisema njia hiyo haiwezi kuwa suluhisho la tatizo la miundombinu. Amesisitiza kuwa wamiliki wa malori wako tayari kuyapaki katika maeneo maalumu iwapo Serikali itawapatia maeneo mbadala yenye miundombinu inayofaa kwa ajili ya maegesho. Lukumay ameitaka Serikali kukaa mezani na TATOA pamoja na wadau wengine wa sekta ya usafirishaji ili kujadili changamoto hizo na kufikia suluhisho la pamoja, akionya kuwa endapo mazungumzo hayatapewa nafasi na agizo la kuyazuia malori kuegesha litaendelea bila kuwepo kwa maeneo mbadala, TATOA inaweza kuagiza malori kupaki nchi nzima. #ChawamataTV #10KFollowers #Asanteni #DarEsSalaam #Tanzania #Bongo #Habari #HabariLeo #BreakingNewsTZ #TanzaniaNews #BongoUpdates #TzUpdates #TzNews #BongoMedia #MediaTanzania #OnlineTV #TrendingTZ #tanzaniatrending#tanzaniatrending #tanzaniatrendingstory #TanzaniaTre #madeintanzania🇹🇿 #madeintanzan #madeintanzania #SupportLocal #madeintanzaniat #roadto100followersontwitch #madeintanzaniawith #viraltz

CHAWAMATA TV
CHAWAMATA TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Wednesday 19 August 2026 04:17:31 GMT
80326
3016
159
160

Music

Download

Comments

oby.oby25
Oby oby :
Sikuhizi kazi zote zimeachwa. imebaki ya kuyaandama maroli na dereva
2026-08-19 05:10:22
25
ranadhanirajabu
R50 :
Chalamila ataondoka Dar ila malori Dar yapo yatakuja na yatakuwepo sana tu
2026-08-19 04:56:32
42
jahangirsmirza
JAHANGIRsMIRZA💥 :
Uwanja wa SabaSaba hauna faida yoyote ufanywe parking za magari makubwa .
2026-08-19 07:53:04
14
easter.paul0
Easter paul :
yaani hii haiko sawa yaani mmesema hata gari ikiharimbika mimi dereva mnaniweka ndani hakuna dereva anayependa gari iharimbike huu uonevu.Ait wakati nasoma mwalimu alisema gari ikiharimbika ninamda wa kutengeneza masaa sabini na.mbili ikiwa haijapona tanirondi waje wanipe msaada.pia sehemu ya kupaki maeneo hamjatuwekea hapo sasa watu watauana naomba mliagaliye kwa kina serekali visasi vitakuwa vingi mimi unanikamata unaniweka ndani kisa nimepaki barabarani familiya yangu itaishije mimi ni dereva hii kauli italeta taharuki
2026-08-19 05:41:24
7
kebby2417
kebby :
Tugome tu madereva watajua umuhimu wetu!
2026-08-21 23:03:17
1
mbekso
user126157407468 :
Tz sio nchi pekee yenye bandari. wengine mbona hawana malori barabarani
2026-08-19 11:38:04
0
user9166239771618
user9166239771618 :
magufuli alilijua haya akatujengea bandali kavu kule Kwara amekufa hawataki TUPAKILIE kule
2026-08-19 05:36:02
6
userjohntruckdriver
JOHN TRUCK DRIVER 🇹🇿 :
Yeah Nikweli ama vipi madereva tunapark magari
2026-08-22 16:43:33
1
zenombele
mbunge2030 :
wakipaki ovo ovo hao tutailalamikia tena serikali
2026-08-19 07:09:32
1
joel.master5
Joel master :
kiongozi Fanya maamuzi sahihi bila kukulupuka kuna maisha baada ya ukuu wa mkoa
2026-08-19 07:19:36
1
ibrahimmwinuka406
Dr Ibrah :
ila Dodoma kazi yake Nini na dar sindio bandari nani inatakiwa ahame dar
2026-08-19 04:54:47
6
mbwanziedsoni
Manu makoko :
sawa baba selikali inakulupuka
2026-08-19 06:13:35
2
user9390028088547
user9390028088547 :
Hbr za kazi mkuu mm naomba kuuliza swali je foleni insababishwa na Wenye Malori.Serikali au ICDs?
2026-08-19 04:47:52
0
lmma.the.boy6
imma mkindi :
huu ni mji wa kiuchumi serekali iende dodoma
2026-08-19 09:44:12
1
zuberi.malota
farhiya zubery :
mpaka polisi wanategea maloli wanatusumbua balabalani
2026-08-19 05:03:53
3
josephkamili.gwan
Jose Paroko :
bandari inahamaa ....ukiwa na maana ya kwamba tukiwa kwala hiyo jamu unakuta wapi ? je wenyew aside ni nani hapo mjini
2026-08-19 04:40:30
1
mbekso
user126157407468 :
babuuu ishu sio hiyo. issue ni malori yasipaki barabarani.
2026-08-19 11:35:07
1
easter.paul0
Easter paul :
naomba matajili kwa hili mlikemee madereva wanatuonea sana harafu maroli ndo yanayotengemewa namkumbuka magufuri kipindi daraja la kiengeya ukitoka dumila lilisombwa na maji akasema lishuhulikiwe haraka maroli yaaze kupita.
2026-08-19 05:48:11
1
victoria.gl20
Victoria GL :
Nyerere alitabiri Kuna siku tutakuwa na kiongozi mwehu, hivi kwanini tusichonge barabara kutoka kigamboni mikwambe hadi vikindu na kutokeza kibaha picha ya ndege, hii itafanya maroli yakitoka bandarini kilwa road na kupita kigamboni Hadi kibaha picha ya ndege hutaona roli mjini
2026-08-22 21:24:10
0
cadabra548
cadabra :
nikupaki tuh akuna kingine maana madereva asaiv atuna samani yeyote Tanzania
2026-08-24 13:44:15
0
nizarkhan8502
Nizar Khan850 :
Ondoeni icd mjini, pelekena kwale kwa magufuli alipo tengeneza. Toa mjini icd.
2026-08-25 22:33:26
0
adam.juma25
hatunaga namba AD :
wagometu maana dah
2026-08-23 18:39:13
0
amirielinazi40
LAST BORN :
wahini hoyeee😅😅
2026-08-23 17:56:44
0
nhegile
baba paroko :
tukopamoja
2026-08-23 07:18:23
0
mwinjiristjcenoso
sparkrapper 👊😜 :
ni kweli kabisa akuna parking DSM
2026-08-19 05:01:39
0
To see more videos from user @chawamata_tv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About