@matibabuimaraclinic: NAMNA YA KUTUMIA CALENDAR KAMA NJIA YA UZAZI WA MPANGO KWA MWANAMKE MWENYE MZUNGUKO WA SIKU 30 Kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 30, unaweza kufuatilia siku zako kwenye kalenda kwa kuhesabu kuanzia siku ya kwanza ya hedhi hadi siku ya 30. SIKU 1–5: HEDHI Hizi ni siku ambazo mwanamke anapata hedhi. Ni mwanzo wa mzunguko mpya. SIKU 6–11: SIKU SALAMA KWA MAKADIRIO Kwa kalenda hii, siku hizi zinawekwa kama siku zenye uwezekano mdogo wa kupata mimba. Hata hivyo, ovulation inaweza kubadilika kutoka mwezi mmoja hadi mwingine. SIKU 12–19: SIKU ZA HATARI (FERTILE WINDOW) Hizi ndizo siku zinazochukuliwa kuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kupata mimba. Mwanamke anayepanga kuzuia mimba anapaswa kuepuka ngono bila kinga katika kipindi hiki au kutumia kondomu. SIKU 20–30: SIKU SALAMA KWA MAKADIRIO Kwa mzunguko huu wa siku 30, siku hizi huwekwa kama kipindi cha uwezekano mdogo wa kupata mimba. Kama kuna sehemu haujaelew andika "nieleweshe". KWA MAWASILIANO NA USHAURI NAMABA YA SIMU +255756718668 #foryou #fyp #trending #tiktok #viral