@skipper4747: Mambo 5 ya kukagua kabla ya kununua gari la used. 1. Angalia engine. Washa gari na uisikilize. Engine inapaswa kufanya kazi kwa utulivu bila kutoa sauti zisizo za kawaida au moshi mwingi. Moshi mweupe au wa bluu unaweza kuashiria tatizo la engine ambalo linaweza kukugharimu pesa nyingi kulirekebisha. 2. Kagua gearbox. Badilisha gear kutoka P kwenda D, kisha D kwenda R. Gear inapaswa kushika haraka bila kuchelewa au kutetemeka. Gearbox yenye hitilafu ni mojawapo ya matengenezo ya gharama kubwa. 3. Hakikisha AC inafanya kazi vizuri. Washa AC kwa dakika chache. Ikiwa haipozi vizuri au inatoa harufu mbaya, inaweza kuhitaji matengenezo ambayo mara nyingi huwa na gharama kubwa. 4. Kagua body ya gari. Angalia kama rangi imefanana kila sehemu na kama milango, boneti na buti zinafungwa vizuri. Tofauti kubwa za rangi au nafasi zinaweza kuonyesha kuwa gari liliwahi kupata ajali. 5. Fanya test drive. Usinunue gari bila kuliendesha. Ukiendesha utaweza kugundua matatizo ya engine, gearbox, brakes na suspension ambayo huenda yasijionyeshe gari likiwa limesimama. Kumbuka: Ukishindwa kujiridhisha na hali ya gari, nenda na fundi mwenye uzoefu kabla ya kufanya malipo. 0670907074 NIPO DARESALAAM TANZANIA.

skipper🤫
skipper🤫
Open In TikTok:
Region: TZ
Wednesday 19 August 2026 08:21:31 GMT
604
8
1
0

Music

Download

Comments

zonza05
Noel Kasonso :
🥰🥰🥰
2026-08-19 15:05:17
0
To see more videos from user @skipper4747, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About