@veriafya: Dkt. Diwani Msemo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) anaeleza kuwa saratani haina umri na inaweza kumpata mtu yeyote, kuanzia watoto hadi watu wazima, huku visababishi vyake vikuu vikiwa ni mtindo wa maisha usiofaa kama vile uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe kupindukia, ulaji wa vyakula visivyofaa na ukosefu wa mazoezi. Pia anafafanua kuwa saratani nyingine kama ya shingo ya kizazi husababishwa na maambukizi ya virusi vya HPV, na anaihimiza jamii kuondoa dhana potofu dhidi ya chanjo iliyowekwa na serikali kwa mabinti wa miaka 9–14, huku akiwasisitiza wanawake waliovuka umri huo kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kubaini na kutibu tatizo hilo mapema. Ameyasema haya leo Agosti 19, 2026 akizungumza na Waaandishi wa Habari Jijini Dodoma, Kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo iliyopo kwenye Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Veriafya
Veriafya
Open In TikTok:
Region: TZ
Wednesday 19 August 2026 09:01:58 GMT
1984
58
1
8

Music

Download

Comments

toy42198
Toy :
😁😁😁
2026-08-19 12:50:40
0
To see more videos from user @veriafya, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About