@veriafya: Dkt. Diwani Msemo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) anaeleza kuwa tafiti za kisayansi zinaonesha maziwa ya mama kuwa na kinga dhidi ya saratani ya matiti, hivyo anawahimiza kina mama kunyonyesha watoto wao badala ya kutumia maziwa ya kopo kwa sababu za kurembesha au kulinda muonekano wao. Ingawa kunyonyesha kunatoa kinga, anaweka wazi kuwa saratani inachangiwa pia na mambo mengine kama vile kurithi (vinasaba), mazingira, na aina ya chakula. Zaidi ya hayo, anafafanua kuwa kina baba pia wanaweza kupata saratani ya matiti (ingawa ni takriban 2% pekee ya visa vyote) na wakiona uvimbe wanapaswa kutafuta matibabu mapema, kwani njia za tiba kama vile kemikali na upasuaji ni sawa na zile zinazotumiwa kwa kina mama Ameyasema haya leo Agosti 19, 2026 akizungumza na Waaandishi wa Habari Jijini Dodoma, Kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo iliyopo kwenye Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Veriafya
Region: TZ
Wednesday 19 August 2026 11:21:16 GMT
Music
Download
Comments
There are no more comments for this video.
To see more videos from user @veriafya, please go to the Tikwm
homepage.