@ommyfitness: Sipo kusambaza hofu ila ni kuwakumbusha kuizingatia sana afya yako. Hawa wamechanganyikiwa kwa kushindwa kumuda gharama za Dialysis - Figo zimefeli. Japo mara moja au mbili kwa mwaka weka utaratibu wa kufanya check-up juu ya Presha ya damu, sukari ya damu, sukari ya seli na ufanyaji kazi wa Figo. Kuna muda utafika hata ukibadilisha mtindo wa maisha utakuwa umeshachelewa. Simaanishi uwe mtu wa diet kama Mimi, namaanisha acha kufanya vitu kwa makusudi. Hili suala sio la kukemea na kusema "Mungu niepushie mbali" ni suala maandalizi. Bahati mbaya wengi wanahisi haiwezi kuwafikia wao. Mwenyezi Mungu Mtukufu awarahisishie safari wote wanaopambana na ugonjwa wa figo, awape wale wanaohangaika kumudu gharama za matibabu, na atulinde dhidi ya magonjwa ambayo hatuyaoni yanavyokuja. Tafadhali, chukulia afya yako kwa uzito. Kuumwa ni kubaya sana. . #ommyfitness #trainerwataifa #KidneyHealth #KidneyDisease #kidneyfailure