@veriafya: Dkt. Diwani Msemo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) anafafanua kuwa saratani ya shingo ya kizazi ndiyo inayoongoza kwa visa na vifo miongoni mwa wanawake nchini (ikichangia takriban 34% ya saratani zote za wanawake), ingawa ni ugonjwa unaoweza kuzuilika kwa chanjo na kuponywa kwa 100% ukibainika mapema katika hatua za mwanzo kupitia uchunguzi. Anataja pia aina nyingine kuu za saratani zinazoongoza nchini katika miaka 30 iliyopita, zikiwemo saratani ya matiti, saratani za mfumo wa chakula (tumbo na utumbo mpana), na saratani ya tezi dume kwa wanaume. Kuhusu kuongezeka kwa wanaougua katika Kanda ya Ziwa, anafafanua kuwa kanda hiyo ina idadi kubwa ya watu ikilinganishwa na maeneo mengine. Ameyasema haya leo Agosti 19, 2026 akizungumza na Waaandishi wa Habari Jijini Dodoma, Kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo iliyopo kwenye Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Veriafya
Region: TZ
Wednesday 19 August 2026 12:22:48 GMT
Music
Download
Comments
poshy_collection :
mbon hawasemi chnzo why kanda ya ziwa na saratani?
2026-08-24 18:53:28
0
kushaa## :
Chanzo chake ni nini?
2026-08-19 14:13:36
0
shufaayasini :
Kwa nini kanda ya ziwa ndo inaongoza kwa saratani ya shingo ya kizazi?? kuliko mikoa mingine??
2026-08-19 17:13:37
0
Magreth venance :
mungu utulinde
2026-08-21 05:38:56
0
Shanelpeterz :
chanzo ni kipi ?na kwanini ipo zaidi Kanda ya ziwa zaidi ?
2026-08-19 15:28:20
0
Ninael :
mko wapo
2026-08-19 18:09:33
0
violeth :
kwanini Kanda ya ziwa iongoze?
2026-08-20 09:32:47
0
user96801627700008 :
nilipokuwa form 3 alikuja doctor kutuchoka chanjo ya saratani ya kizazi ila ilikuwa na kuwa na Miaka 14-15 mkoa wa Kagera
2026-08-20 04:19:01
0
Mariam Moha :
wanaume.wapewe elimu piaa,maana wanabeba hcho kirusi kutoka kwa mwanamke mwingine kwenda kwa mwanamke mwingine,watu muwe waaaminifuu kwa wenza wenu,muwe na huruma hofu ya Mungu
2026-08-20 05:09:16
1
To see more videos from user @veriafya, please go to the Tikwm
homepage.