@abdillah_nyonje: Leo, tarehe 19 Agosti 2026, nimepata heshima na bahati ya kutembelewa na msanii mkongwe wa muziki wa Taarab Zanzibar, ndugu Abdalla Issa. Ziara hii ilikuwa na lengo la kubadilishana mawazo, uzoefu na kupokea ushauri kuhusu namna bora ya kusimamia na kuendeleza kazi za sanaa kupitia muziki, hususan katika kuhakikisha kuwa wasanii waliotumia vipaji na ubunifu wao katika kutengeneza kazi mbalimbali za muziki wanaendelea kunufaika na kazi zao. Ninathamini sana uzoefu, hekima na mchango wa wasanii wakongwe katika maendeleo ya sanaa Zanzibar. Ushirikiano na mazungumzo ya aina hii ni muhimu katika kujenga mifumo bora ya kulinda, kusimamia na kukuza kazi za wasanii kwa maslahi mapana ya sekta ya sanaa na kizazi kijacho. Asante sana ndugu Abdalla Issa @abdallaiss kwa ziara, mawazo na ushauri wako muhimu.
Lahy Nyonje
Region: TZ
Wednesday 19 August 2026 13:57:04 GMT
Music
Download
Comments
Eddy :
Ustadh hataki music delete please
2026-08-31 20:12:07
0
Shufaina Khamis :
🤩🤩🤩
2026-08-20 05:31:11
0
To see more videos from user @abdillah_nyonje, please go to the Tikwm
homepage.