@dianafemhealth: PCOS siyo tu tatizo la hedhi. 🌸 Kuna wanawake wanaishi na dalili mbalimbali bila kujua kwamba zinaweza kuhusishwa na PCOS — kama vile hedhi kutokuwa na mpangilio, chunusi nyingi, kuongezeka kwa nywele usoni au mwilini, nywele za kichwani kupungua, kuongezeka uzito, mabaka meusi kwenye ngozi au kupata changamoto ya ujauzito. PCOS inaweza kuathiri mfumo wa homoni na namna mayai yanavyokomaa na kuachiliwa, hivyo kwa baadhi ya wanawake inaweza kufanya ovulation isiwe ya kawaida. Lakini muhimu zaidi ni kutotazama dalili moja pekee na kujihitimishia kuwa una PCOS. Utambuzi unahitaji tathmini ya kitaalamu na vipimo vinavyofaa. 👉 Je, una mojawapo ya dalili hizi? Andika “PCOS” kwenye comment nikueleze hatua za kuanza kuchunguza chanzo. #ohio #kentucky #losanges #usareeles
DianaFemHealth
Region: TZ
Wednesday 19 August 2026 17:05:42 GMT
Music
Download
Comments
There are no more comments for this video.
To see more videos from user @dianafemhealth, please go to the Tikwm
homepage.