@veriafya: Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi, Daniel Michael anaeleza kuwa uvimbe kwenye kizazi unaweza kumfanya mwanamke ashindwe kupata ujauzito kulingana na ukubwa, idadi na sehemu uvimbe ulipokaa, ingawa si wanawake wote wenye uvimbe wanaopatwa na tatizo hilo. Aidha, anaeleza kuwa mwanamke anaweza kupata ujauzito akiwa na uvimbe, lakini mtoto na uvimbe hushindania mzunguko wa damu kwenye kizazi, jambo linaloweza kusababisha mimba kuharibika au mwanamke kupata maumivu makali wakati wa ujauzito. Video nzima ipo kwenye YouTube chaneli yetu inayopatikana kwa Jina la Veriafya