@mboya_the_great: MTAKATIFU WA LEO Alhamis, August 20, 2026 *Mtakatifu Bernard, Abate na mwalimu wa kanisa* Mtakatifu Bernard alizaliwa mwaka1090, huko Fountaine-les-Dijon,Ufaransa. Alizaliwa katika familia iliyoheshimika sana.Alisoma pia katika shule bora,na alipenda pia masomo ya Biblia. Mwaka 1111,Mtakatifu Bernard na vijana wengine 30, walijiunga na monasteri ya Citeaux, ambayo ilikuwa chini ya Wa Benedictine. Mwaka 1115 ,Mtakatifu Bernard na wenzake 12, walienda kuanzisha monasteri mpya ya Clairvaux. Naye akachaguliwa kuwa Abate,na katika kipindi kifupi, walipokea vijana 130, ambao walijiunga nao . Mtakatifu Bernard alikuwa karibu na Askofu William wa Champeaux. Kutokana na wingi wa watawa,mwaka 1118, Mtakatifu Bernard alituma watawa kwenda kuanzisha monasteri huko Chalons. Kutokana na busara na hekima zake, Mtakatifu alitumika kutatua matatizo katika kanisa katika ngazi zote.Alipata muda pia wa kuandika nyaraka mbalimbali,aliwaelewesha na kuwafundisha pia wapinga Kristo. Mtakatifu Bernard aliendelea pia na uinjilishaji,akatuma watawa katika nchi mbalimbali za Ulaya. Mtakatifu Bernard alikufa mwaka 1153 August 20 huko Clairvaux Ufaransa.Alitangazwa Mtakatifu mwaka 1174 Januari 18 na Papa Alexander III *Watakatifu wengine wa leo ni* Mt. Amadour Mt. Baamin Mt. Bernard wa Valdeiglesias Mt. Edbert Mt. Haduin Mt. Heliodorus Mt. Herbert Hoscam Wt. Leovigild na Christopher Mt. Lucius Mashahidi wa Thrace Mt. Maximus Mt. Philibert Mt. Ronald *Mtakatifu Bernard na Wenyeheri na Watakatifu wengine wote wa leo, Mtuombee*
Mboya Regan
Region: TZ
Thursday 20 August 2026 08:53:11 GMT
Music
Download
Comments
traole👺💀 :
😁😁😁
2026-08-21 04:42:25
0
To see more videos from user @mboya_the_great, please go to the Tikwm
homepage.