@madininews: Jengo la Kanisa la Victory Gospel Assembly lililopo chini ya Askofu Paulo Shemsanga limebomolewa kufuatia mgogoro wa muda mrefu wa uwanja kati ya familia ya Mzee Wilfred Mwankuga Mwanjala na Askofu Shemsanga, katika Kiwanja Namba TMK/KEKOMAGURUMBASI A2/122 kilichopo Mtaa wa Magurumbasi A, Kata ya Keko, Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam. Familia ya Mzee Wilfred Mwankuga Mwanjala inadai kumiliki hati halali ya makazi ya eneo hilo yenye namba TMK002389, ikisisitiza kuwa ubomoaji huo umeendeshwa kwa mujibu wa sheria kufuatia kushindikana kwa mashauriano na makubaliano ya awali kati yao na uongozi wa kanisa hilo. Akifafanua chanzo cha mgogoro huo, Elisha Wilfred, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Mzee Wilfred, ameeleza kuwa familia yao ilinunua eneo hilo mwaka 1991 na baadaye baba yake alimkaribisha Mchungaji Paul Shemsanga kutumia kiwanja hicho kwa ajili ya ibada kukiwa na makubaliano maalum kufuatia kanisa kukosa eneo. Hata hivyo, Elisha amebainisha kuwa mwaka 2002 Mzee Wilfred alisitisha makubaliano hayo kwa barua rasmi na kumtaka Askofu Shemsanga kurejesha eneo hilo lakini halikurejeshwa. Ameongeza kuwa hata jitihada za maridhiano zilizofanyika tena mwaka 2019 hazikufanikiwa kutokana na upande wa kanisa kukiuka masharti, hatua iliyomfanya baba yake kuchukua mkondo wa kisheria ili kurudishiwa eneo lake. Kwa upande wake, mchungaji wa kanisa hilo, Mch. Flora V. Shemsanga, ameeleza kuwa walipata taarifa za watu kufika katika eneo la kanisa usiku wa kuamkia Agosti 18, 2026 wakiwa na zana za ubomoaji, wakisindikizwa na walinzi wa kampuni binafsi. Amesikitishwa na hatua hiyo huku akidai kuwa upande wa kanisa haukuoneshwa kibali chochote cha Mahakama wala wakili wao kushirikishwa kwenye shauri lolote lililoamuru kuondolewa kwao.#view ##tranding #tiktoktanzania🇹🇿
MADINI TV
Region: TZ
Thursday 20 August 2026 13:59:30 GMT
Music
Download
Comments
Mama t :
BABA ULITOA NAJUA UMESHAWISHIWA NA WATOTO MUNGU NISAIDIE KUTOSIKILIZA SAUTI ZA WATU.AU WATOTO WATABADILISHA JATA MOYO WAKO.
2026-08-21 04:43:20
0
𝓓𝓮𝓫𝓻𝓪𝓲𝓷 𝒅𝒕𝒄324 :
hapa ni wapiiii
2026-10-29 17:58:45
0
Aunt :
Sasa wao siwangenunua kiwanja, walitaka kumzulumu baba
2026-11-03 05:43:10
2
Loading :
Good
2026-10-31 08:23:24
0
MKEREWE FINEST💎 :
hapo kunamambo haya✌️
2026-10-22 16:52:38
1
Betty Mbone :
wee mungu atete nao
2026-10-29 17:05:37
0
benjamin kasisi :
MUNGU MTENDA HAKI ATASHUGHULIKIA TENA KWA HAKI HAKI ATAITOA
2026-11-01 17:23:19
0
Basanga :
jamani mmmmhi
2026-08-22 11:37:10
1
user4694971199906 :
mhh kaz ishakuwa ngumhuku
2026-08-21 02:41:17
0
it's i S.. :
khaaa
2026-10-28 16:13:45
0
Loading :
Goood
2026-10-31 08:23:21
0
Humutu :
Shida ya kupeana vitu kiholela
2026-08-20 19:45:40
1
Emasoni Hemed :
mwamposa abomolewa kanisa
2026-10-29 08:18:43
0
Juma Msati :
Nimefulai babu kupata haki yake mungu mkubwa sana,kanisa la kiwanja cha zuluma kuvunjwa
2026-08-23 13:05:35
0
muddi boy :
acheni kuzulum wachungaji acheni wizi
2026-10-30 17:41:43
0
☆GWEJU TV☆ :
USIJARI KANISA SIO LAKO KANISA LA YESU KRISTO NA YEYE USIULIZE YESU YUKO WAPI? YESU MWENYEWE YUKO HAPO MTAA WA PILI ANAKUJA USIWAZE, NI WATU GANI WAVUNJAO KANISA LA HUYU JAMAA AU KANISA LIMEJENGWA KWENYE ENEO LISILO SAHIHI KUJENGWA?
2026-11-05 21:28:57
0
Sweetgirl💕...tz🇹🇿 :
Nayapaje Ayo mabati jaman 🤣🤣🤣🤸
2026-10-29 03:19:30
0
Adv_NKWERA :
🔥
2026-08-21 05:21:28
1
Sakaya Lobebeki :
😁😁😁
2026-08-25 07:52:18
0
SAFARI WA KUNYUMBA :
🙏
2026-11-08 15:57:32
0
To see more videos from user @madininews, please go to the Tikwm
homepage.