@mkerewemedia: Jeshi la Polisi Mkoani Geita limempongeza Mwenyekuti wa Halmashauri ya wilaya ya Geita na Diwani wa kata ya Ludete , Jumanne Misungwi kwa ushirikiano ambao amekuwa akiutoa kwa Jeshi hilo katika kuhakikisha wanaokoa vijana ambao wamekuwa wakijiingiza katika magenge ya Uharifu na badala yake kuanzisha matamasha ambayo yamekuwa chachu kwa vijana ndani ya Mamlaka ya Mji mdogo wa katoro. Hayo yamesemwa na Kamanda wa polisi Mkoa wa Geita , SACP. Safia Jongo katika kuelekea Maadhimisho ya Miaka 20 ya Polisi Jamii wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mamlaka hiyo sambamba na kuwahasa wananchi kuendelea kuitunza amani ya Mkoa wa Geita .