@kelseymalaika: 🍓 STRAWBERRY CAKE FILLING — PART 1 OF 2 Huna fresh strawberries? Unaweza kutengeneza strawberry filling tamu sana kwa kutumia jam tu! Kikombe 1 cha strawberry jam (1 cup) Kijiko kikubwa 1 cha juice ya limao (1 tbsp) Kijiko kikubwa 1 cha corn flour (1 tbsp) Vijiko vikubwa 2 vya maji (2 tbsp) Nusu kijiko kidogo cha vanilla (½ tsp) Chumvi kidogo Weka jam na juice ya limao kwenye sufuria, ipashe kidogo (low heat). Pembeni changanya corn flour na maji, halafu mimina kwenye jam huku unakoroga. Endelea kupika na kukoroga kwa dakika 3-5 mpaka iwe nzito kidogo. Malizia na vanilla na chumvi kidogo, then acha ipoe kabisa. Unaweza kuitumia kwenye cakes, cupcakes au dessert yoyote unayotaka. Save recipe hii! Part 2 tutatumia fresh strawberries! 🍓 #daressalaam #tanzania #livingintanzania #jinsiyakupikakeki #lifeabroad @The Cake Edit TZ