@nyayotv: Mwanafunzi wa kidato cha sita, Peter Maira (23), wa Shule ya Sekondari Makongoro, Bunda mkoani Mara, anadaiwa kupigwa viboko na walimu kwa kosa la kufeli mitihani hadi kupoteza uhai wake. Tukio hilo linadaiwa kutokea Agosti 19, 2026, ambapo mwanafunzi huyo alipelekwa hospitalini akiwa katika hali mbaya na baadae alifariki. Jeshi la Polisi mkoani Mara limewakamata walimu sita kwa ajili ya uchunguzi kuhusu tukio hilo huku uchunguzi wa mwili wa mwanafunzi huyo ukifanyika ili kubaini chanzo Cha kifo chake. Follow us 🙏 #fyp #creatorsearchinsight #fypシ゚viral #tiktoktanzania🇹🇿 #tiktokkenya