@ktnnewske: Mbunge wa Homa Bay Mjini Peter Kaluma na baadhi ya viongozi kutoka kaunti hiyo wameonekana kuhatarisha usalama wa taifa kwa matamshi yao. Jumapili, wakati wa mkutano wa vuguvugu la Linda Mwananchi huko Homa Bay, vurugu zilizoonekana kupangwa zilisababisha vifo vya watu wanne, huku makumi ya wengine wakiuguza majeraha mabaya na mali kuharibiwa. Kaluma na Gavana wa kaunti hiyo Gladys Wanga wakitajwa pakubwa katika mzunguko wa matukio hayo. #DiraYaWiki