@kambi_health: “WAPO UNAMALIZA KULA, KIFUA KINAANZA KUWA MOTO?” 🔥 Kama baada ya kula unahisi kifua kinawaka moto, chakula au tindikali inapanda kooni, mdomo kuwa na uchachu au unapata kubanwa kifuani, usipuuze hali hiyo. Mara nyingi hali hii huhusishwa na acid reflux (GERD) — ambapo tindikali iliyopo tumboni hurudi juu kuelekea kwenye umio na kusababisha ile hali ya kuungua. Lakini swali muhimu ni: kwa nini inatokea zaidi baada ya kula? Unapokula, tumbo hujaa na kuzalisha tindikali kwa ajili ya mmeng’enyo wa chakula. Ukila chakula kingi, kula kwa haraka, kulala muda mfupi baada ya kula, au kutumia vyakula vinavyochochea reflux kwa mwili wako, tindikali inaweza kurudi juu kwa urahisi zaidi. 👉 Ndiyo maana kutibu dalili pekee bila kuelewa kinachosababisha kurudia kwake kunaweza kukufanya uendelee kupata tatizo mara kwa mara. Anza kwa kuangalia aina na kiasi cha chakula unachokula, muda wa kula, na tabia zako baada ya kula. Kifua kuwaka baada ya kula si kitu cha kuzoea tu—uelewe chanzo chake. ❤️‍🩹 #AcidReflux #Kiungulia #AfyaYaTumbo #Mmomeng’enyo #drkambi

KAMBI  HEALTH ||
KAMBI HEALTH ||
Open In TikTok:
Region: TZ
Friday 21 August 2026 20:11:00 GMT
1592
22
0
2

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @kambi_health, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About