@veriafya: Akishauri kupitia Mwananchi Digital Mfiziotherapia Emmanuel Jacob kutoka Taaasisi ya Mifupa - MOI ameshauri kuwa mtu anapokaa ahakikishe makalio yamegusa mwisho wa kiti ndipo aegemee ili kuepuka mkao mbaya unaoweza kusababisha maumivu ya mgongo. Pia mikao kama ya kukunja nne, kulalia kiti au kuegemea meza kwa muda mrefu ni mibaya kwa afya ya mgongo na inapaswa kuepeukwa.