@official_papaambalamwezi: CHANJO YA NEWCASTLE YA VIFARANGA VYA SIKU 7 NI TOFAUTI NA YA SIKU 21 UKICHANGANYA UTAKUWA HUJATOA CHANJO wengi wetu tunachanganya hizi chanjo mbili kwa sababu zote ni za Newcastle. Siku ya 7: Mara nyingi hutumika Newcastle HB1 kuanzisha kinga kwa vifaranga na sawa na Mtoto mdogo kumpa maziwa sio ugali hivyo usimpe kifaranga wa siku 7 chanjo ambayo ulitakiwa kumpa wa siku 21 Siku ya 21: Mara nyingi hutumika Newcastle LaSota kama booster ya kuimarisha kinga. Hivyo ukimpa HB1 ambayo ulitakiwa kumpa kifaranga cha siku 7 haitakuwa vizuri ni sawa na kumlisha mtu mzima anaelima uji wa mtoto Kwa hiyo, HB1 ya siku 7 na LaSota ya siku 21 si kitu kimoja kwenye ratiba ya chanjo. Usiangalie jina “Newcastle” pekee. Angalia aina ya chanjo na siku inayotakiwa kutolewa. Ukichanganya ratiba, unaweza kudhani umewapa chanjo wakati ratiba yako haijakamilika vizuri. #chanjoyanewcastle #ufugajiwakuku #vifarangavyakuku @highlight

SAVANA KUKU FARM
SAVANA KUKU FARM
Open In TikTok:
Region: TZ
Monday 24 August 2026 09:58:32 GMT
5940
193
3
39

Music

Download

Comments

user5705470093762
user5705470093762 :
Mhhh nichanhanyikiwa sasa. Na mbona sijawahi kujua hii kitu jamani😇
2026-08-24 12:00:40
0
epie018
Epie018 :
Duuuu
2026-08-24 19:47:03
0
To see more videos from user @official_papaambalamwezi, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About