@bongo_media: Leo, Agosti 24, 2026, mume wa Sharifa, Tariq Abdallah amesema alipokea simu kutoka Kituo cha Polisi Chanika na kuambiwa kuwa kuna mtu aliyefikishwa kituoni hapo kwa tuhuma za kuhusika na 'wizi' wa mtoto. Tariq amesema alipofika aligundua kuwa mtoto aliyekuwa akihusishwa na tukio hilo alikuwa mwanawe, Amayra, ambaye alipotea takribani mwezi mmoja na nusu uliopita. Kwa mujibu wa taarifa za awali zinazohusiana na tukio hilo, inadaiwa kuwa mtuhumiwa alimchukua mtoto huyo akambadili jina kwa lengo la kumdanganya mwanaume wake anayeishi Songea akidai kuwa alikuwa mjamzito na baadaye amejifungua. Taarifa za kuaminika ni kuwa mtuhumiwa anashikiliwa Kituo cha Polisi Chanika, huku jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, ACP Yustino Mgonja au Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Muliro Jumanne Muliro zikiendelea.
BONGO MEDIA
Region: TZ
Monday 24 August 2026 17:56:05 GMT
Music
Download
Comments
Kidachiistore :
Ila mwizi kamtunza jaman kitoto Kina afya 🥰
2026-08-24 19:30:30
512
Edina Chami :
ila mwizi alijuwa kumtunza mtoto🥰🥰🥰 i love u mwizi baby
2026-08-24 20:27:48
319
Jackie😍 Jackline :
Em ngoja kwanza Ko mwizi kamuita mtoto jack 😅
2026-08-24 19:46:36
100
shija Juma :
mwizi kamtuza mtt jamn nae mungu amsaidie apate wake
2026-08-25 07:10:58
130
ATIENO❤️ :
Kamenenepa mashaallah🥰🥰🥰🥰🥰 mwizi mitano tena Ila kwangu usiguse😂😂😂
2026-08-25 09:14:35
54
Momo D❤️ :
Mungu ni mwema ila ingekuwa vzr hyo baba wa mtoto na mama Watt wamsamehe alimchukua mtoto japo hajatumia njia sahihi lakini anaonekana anafya yake nzuri safi kabsa Allah amjalie mtoto aendelee kukuwa vyema
2026-08-24 18:38:53
64
joyce :
ni yule mtoto alichukuliwa akiwa na sm 40au mwingine
2026-08-24 19:14:36
58
Wema Ismaili :
Kingine chakushukuru amemlea vizuri mana naona anaafya nzuri🙏🙏
2026-08-24 19:00:08
88
💓Brigither doto💗 :
mungu yu mwema kwa hiyo ataendelea kunyonyesha🥰
2026-08-24 19:08:29
24
Jordinlee :
Kim ukweli huyo mwizi hakuwa na nia mbaya☹️mtt Yuko vizuri mno, wamsamehe tu🙏
2026-08-25 06:51:26
17
ummu ilham😘 :
hapo sahiv hamwamini yoyote
2026-08-24 18:47:37
36
MissOli👩🦰💞 :
aliyeiba mtoto kafariki inauma sana sijuw nini kilimpata adi akaiba mtoto atimae kafariki inauma jamani 😭😭😭😭
2026-08-25 11:12:01
7
Muhammad Nguja. :
Mmeiyona kazi ya serikali?
jitihada za serikali kama hizi hatuzioni,
ila serikali ikiteleza kidogo tu tena kwa baadhi ya watumishi,
basi tunaanza kuitukana serikali yote mpama raisi.
2026-08-24 20:48:48
10
user178736737730 :
kwani mwizi anasemaje hebu tupate maoni yake
2026-08-25 06:16:39
9
kipepeo1 :
Mimi ningeunga urafik na mwizi hata wa maombi 🥺🥺na ningesamehe kabisaa
2026-08-24 20:35:06
6
user9707923226129 :
wamsamehe tu kwa vile alimtunza vizuri tumuombee mungu ampe wake
2026-08-25 08:14:34
7
Shery Rm😍 :
Aisee kwan ilikuaje jaman me ndokwanza naiyona leo hii taarfa,,,Pia hongeren sana mungu ni mwema jaman
2026-08-24 20:09:21
9
aziza :
ALLAH NI MWEMA ILA SALINI SUNNA SALA TUL SHUKRAN MUMUOMBEE DUA HUYO MTOTO ALLAH AMVUE HILI NA JENGINE
2026-08-24 19:24:30
14
Official Runa Ngwambe :
mimi sina mtoto siwezi kuiba mtoto wawatu wala sitamani mtoto wamtu nitalea watoto wandugu akikua atarudi kwao
2026-08-25 05:39:42
11
lightzuu :
ila aliemchukua alimlea vizuri sana
2026-08-24 19:32:31
13
user3156966988261 :
Huyo mwizi kampenda mtoto Kam chukuwa kwa kiroho Safi maskini Allah ampe nayeye riski ya mtoto maskini watu wanatafuta watoto mtu ukipata mimba iwe kwa shida au kwa raha jamani
2026-08-25 06:14:28
7
Veronica Daudi :
alhamdulillah amepatikana jamani mungu ni mwema kila wakati nimefulahi utazani uyo mtt namjuwa mw/mungu awakuzie
2026-08-24 18:36:15
25
user9621459481693 :
mwizi apewe tuzo mtoto mashaallah
2026-08-24 19:48:59
9
ney chazy :
Duuuuh mwiz alikuwa na Nia njem jomn msamehn tu mtot kapendz kweli 😳
2026-08-24 20:01:56
5
Sarah :
Mungu mwem
2026-08-24 18:27:30
6
To see more videos from user @bongo_media, please go to the Tikwm
homepage.