@binti_waamani: Kufanya vitu vichache kwa ajili ya Allah ni bora zaidi kuliko vingi kwa ajili ya kuvuna sifa za watu. Nyumba yako ya ndoto haiko hapa duniani, ila mwanzo wa kuitengeza iyo ndoto ni hapa duniani. Ili uweze kufaulu, hisia zako zote zinapaswa kubebwa na Allah, ukichukia chukia kwa ajili yake na hata ukipenda penda kwa ajili yake. Muda wako wote ulonao siyo wa kupoteza ni amana na utaulizwa matumizi yake hapo kesho, jitihahada nzuri ni kuona kila sekunde unayotumia ni mbegu na mavuno yake utayaona. #jannah #hijabgirl #mendinghearts #i̇slam #muslima