@tzpanoramadigital: Waziri Mkuu wa Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba, amezitaka mamlaka za mikoa kuhakikisha stendi zilizojengwa kwa ajili ya mabasi zinatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa. Dk. Mwigulu ametoa agizo hilo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha vyuo vikuu, Asha Juma Feruzi. Amesema miundombinu hiyo inapaswa kutumika ipasavyo ili kuhakikisha mabasi na abiria wanapata huduma bora, salama na zenye utaratibu. Aidha, Waziri Mkuu amesisitiza kuwa stendi hizo hazipaswi kubadilishiwa matumizi bila kuzingatia madhumuni yaliyokusudiwa wakati wa ujenzi wake. Ameeleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kulinda uwekezaji wa Serikali, pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata thamani ya fedha zilizotumika katika ujenzi wa miundombinu hiyo.

Tanzania Panorama Online
Tanzania Panorama Online
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 27 August 2026 11:40:56 GMT
5453
121
0
5

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @tzpanoramadigital, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About