@gillybonny_tv: Mwanamke raia wa Ghana, Mercy Yaaba Bredu, amefariki dunia nchini China baada ya kuanguka ghafla kwenye uwanja wa ndege, muda mfupi tu baada ya kuwasili nchini humo kuendelea na masomo ya Digrii ya Uzamili (Master’s Degree). Bredu aliondoka nchini Ghana Agosti 24, 2026, kuelekea China kuanza masomo yake. Hata hivyo, akiwa njiani kwenye ndege, alilalamika kupata maumivu ya kifua na moyo. Baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege nchini China, alidondoka ghafla wakati akipokea zawadi ya maua ya kumkaribisha, jambo lililofanya akimbizwe hospitalini kwa matibabu ya dharura kabla ya mauti kumfika Agosti 26, 2026. Mwanamke huyo, aliyewahi kuhudumu kama Makamu wa Rais wa Chama cha Wanafunzi wa Lugha ya Kiingereza (ASSENS) katika Chuo Kikuu cha Elimu cha Winneba (UEW) mwaka 2024, alikuwa amehitimu digrii ya kwanza kwa ufaulu wa juu wa daraja la kwanza (First-Class Honours). Ufaulu huo ulimwezesha kupata ufadhili wa masomo (scholarship) nchini Marekani na China, ambapo alichagua kwenda China kujiendeleza kimasomo na kibiashara. Ingawa umri wake haukutajwa kwenye taarifa hiyo, kifo chake cha ghafla ndani ya siku mbili tu tangu aagane na familia yake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Accra kimezua simanzi na majonzi makubwa miongoni mwa familia, marafiki na wanachuo wenzake.
Gilly Bonny Tv
Region: TZ
Saturday 29 August 2026 06:35:03 GMT
Music
Download
Comments
Finegirl🌺 :
Village people🥺
2026-08-29 16:12:01
1
God Alone :
move in SILENCE SILENCE SILENCE😢😢
2026-08-30 01:43:16
1
Sally :
Aliwaaga marafiki wa nini
2026-08-29 12:24:57
49
Justin stamphord :
sio kwa ubaya ila ndugu zetu ndio wanaturoga
2026-08-29 16:02:43
86
Madam P :
My country people 🙌🏽🙌🏽🙌🏽
2026-08-29 22:08:42
0
Ms.Aurelia🌸 :
poleni
2026-08-29 12:37:40
0
meda :
watu wanaroga tuwemakini jambo la muhimu la maisha linatakiwa liwe siri
2026-08-29 11:44:03
16
STAR KING FASION STORF :
kweli watu wanaloga
2026-08-29 11:45:34
17
V :
daaah 😭😭 jaman tukumbuke wabaya wetu awatoki mbali ni watu wetu wa karibu na pia vitu vinavotupa fraha tujaribu kuvifanya Siri siyo kila jambo unamwambia mtu vingine tufanye t Siri maan si kila anaekuchekea anafrahia maendleo yako😭
2026-08-29 09:16:32
85
niahgezu :
Ndo maana hua siagi nikisafiri
2026-08-29 17:06:31
9
laoo d mama :
nilijua uchawi upo tz to dah😭😭 Mungu ampokee
2026-08-30 06:10:06
4
Tina kidot :
sio kurogwa tu ata pressure pia ya safari inaweza pelekea kama mm nimuoga sana wa ndege😂
2026-08-29 09:50:09
25
Elune Ritte :
Kalogwaa jmn haiwezekan mtu aondokee mzm afike kafa jmm 😳😳 bila sababu loooh
2026-08-30 04:05:11
2
mkami ndumez 🇰🇪 :
😭😭😭ishawai kumtokea rafiki yangu mmoja peter tambaru mungu mlaze mahara pema
2026-08-29 07:40:24
15
d square🦋 :
MIMI SIAGAGI MTU NACHOMOK KAM USHUZIIII MIJITU YA SIKU HIZI HAIFAI KABS HATA MPENZ WAKO SIYO WA KUMUAGA MIMI WANANIJUA NKIJIAMULIA HAT WAZAZI SIWAAGI🥺🥺🥺
2026-08-29 19:12:57
4
MuuEnosh💞 :
Tatizo linakuja kusimulia kila mtu unachofany daaa tujifunz kuwa wasiri namambo yetu akijua mama na baba inatosha mnoooooo
2026-08-30 06:01:46
1
Ayana😍 :
kwaiyo alikufa akiwa kwenye ndege
2026-08-29 13:52:05
1
Linah John :
Au alipata mshituko ndege ilivotua chini jmn ila mm ilinitokeaga nilisafili kwenda ukweni sikujua sinikaaga kilichonitokea sikusafili nilipewa kamuogo na shangazi wa hapo imefika sa kumi nilitapika na kuhalisha mpaka samoja alafu anisaidii na nipo na wtt wadogo wawili nikawapigia wa kwa mama wakasema watanila nyama mzazi mwezangu akapigiwa cm akaongea na ndugu zake wakachinja kuku nikapewa mchuzi sijui waliweka nn singida sita pasahau nimekoma kuaga mimi mtu akiniuliza nawapiga mwezi kumbe naondoka leo pole yake hapumzike kwa amani
2026-08-29 16:40:57
2
MissOli👩🦰💞 :
ndoman mimi amna mtu anaejuwa atuwa zangu nikweli namtegemey Mungu ila wanadamu kunanamna naishi nao
2026-08-29 16:28:02
5
Miss vee 🦋💕😍 :
Safari ya kwanza ya ndege haitangazwi jmn 😥
2026-08-29 19:42:17
1
Andrew Bracken (Proudly Deaf) :
kutokujitambua tusikilize na wazazi wetu wanachotushaurii na mambo ya ustarehe yapo tu ivi sio vifo Mungu anavyovitaka ni kuletea wazazi kovu la maisha tu kwann mtu tayr una mtoto usiwe na uchungu na yule kiumbe ulie mleta duniani uka take care ukaachana na mambo ya heka heka za dunia jman yaan duuu mm naendelea kujifunza kupitia haya duu
2026-08-29 13:57:56
0
BATA MAJI 🦢 :
Dah 💔watu wachaw san
2026-08-29 16:28:24
0
Blessed Girl 🏹 :
usiri muhimu
2026-08-29 12:29:32
2
Its chuchu🦋❤️ :
Daah
2026-08-29 11:57:43
1
obama obama . :
inaonekana kaagasana mungu amuongoze salama
2026-08-29 09:07:38
2
To see more videos from user @gillybonny_tv, please go to the Tikwm
homepage.