@nuktatanzania: Deogratius Ndejembi sasa ni Makamu wa Rais wa Tanzania baada ya kuapishwa rasmi leo Jumamosi, Agosti 29, 2026, katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan. Ndejembi ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju, ikiwa ni hatua inayokamilisha mchakato wa kumuingiza rasmi katika nafasi hiyo baada ya kuthibitishwa na Bunge jana Ijumaa, Agosti 28, 2026. Kabla ya uteuzi huo, Ndejembi alikuwa Waziri wa Nishati na Mbunge wa Chamwino, Dodoma. Anachukua nafasi hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Dk Emmanuel Nchimbi, ambaye alitangaza kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais na kwamba ataondoka rasmi madarakani Septemba 4, 2026. Kwa kuapishwa kwake leo, Ndejembi anakuwa Makamu wa Rais wa tatu kuhudumu chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, baada ya Dk Philip Mpango na Dk Emmanuel Nchimbi. Aidha, Ndejembi anakuwa mmoja wa Makamu wa Rais wenye umri mdogo zaidi kuwahi kushika nafasi hiyo katika historia ya Tanzania.
NuktaTanzania
Region: TZ
Saturday 29 August 2026 06:54:11 GMT
Music
Download
Comments
Kemmy Rwechungula Francis :
Utukumbuke tulio ktkt ya vituo vya mafuta tunakufa.😭
2026-08-29 07:02:25
0
muya :
hapo nimejifunza kitu ukweli hauaminiki ungo hutukuzwa
2026-08-29 07:15:33
0
To see more videos from user @nuktatanzania, please go to the Tikwm
homepage.