@ngasatvdodoma: ROYAL V SAFARI YAREJEA NA MABASI MAPYA YA KISASA Dodoma: Kampuni ya usafirishaji ya Royal Village Safari, inayotokana na Royal Village Hotels, imetangaza kurejea rasmi katika sekta ya usafirishaji ikiwa na mabasi mapya ya kifahari na huduma za kisasa. Akizungumza kuhusu ujio huo, Boss @melekh_said wa kampuni amesema Royal V Safari si kampuni mpya kabisa, kwani awali walikuwa wakifanya shughuli za usafirishaji kupitia mabasi yaliyokuwa yakijulikana kama Shatco. Amesema tofauti kubwa kwa sasa ni maboresho makubwa yaliyofanyika, ikiwemo ununuzi wa mabasi mapya yenye huduma za kisasa. «“Sasa tumenunua magari mapya kabisa, full luxury. Yana AC, TV, choo, Wi-Fi na cameras. Kwa hiyo mtu akiingia ndani anapata kitu tofauti kabisa na mwanzo,” amesema.» Kwa mujibu wa kampuni hiyo, safari zimeanza huku wakipokea maoni kutoka kwa wananchi waliokuwa wakitaka kujua njia ambazo mabasi hayo yatapita. Kwa awamu ya kwanza, Royal V Safari itahudumia njia zifuatazo: - Kiomboi – Dar es Salaam - Dar es Salaam – Kiomboi - Singida – Dar es Salaam - Dar es Salaam – Singida - Kiomboi – Rombo - Singida – Rombo Kwa upande wa Singida, kampuni imeeleza kuwa kutakuwa na mabasi ya mchana, alfajiri na jioni, huku safari za Kiomboi zikiwa zimepangwa zaidi wakati wa jioni. Kampuni hiyo imeahidi kuendelea kuboresha huduma na kuongeza njia nyingine kadri shughuli zitakavyoendelea. @royalvsafari @melekh_said
Ngasatvdodoma
Region: TZ
Saturday 29 August 2026 07:44:01 GMT
Music
Download
Comments
silayomagarina simu used :
rombo once again
2026-08-29 17:16:33
1
KING SELLA TZ :
shatco one ✨
2026-08-29 18:53:32
0
Aisha Abdull :
Inabidi uweke soft blankets my boss
2026-08-29 14:06:47
0
SADA JUMA :
hongera sana boss wangu haya ndo maendeleo
2026-08-30 09:21:04
2
glory Alfred :
weeeeeeeweeer
2026-08-29 15:30:34
0
jedbil05 :
shatco
2026-08-29 14:33:31
0
Clistina Malinjaga :
naomba kujua, SHABIBY, SATCO NA SHATCO hawa ni ndugu?
2026-08-30 05:20:06
1
mohamedy muya :
Shabibi mdogo yuleeeee
2026-08-30 02:30:38
0
baba_charity :
Wilaya ya Rombo ina basi nyingi kuliko baadhi ya mikoa kwa ujumla aisee
2026-08-29 19:47:00
3
smart boy 06 :
tupeni na sisi moja kondoa masange to DSM
2026-08-29 15:21:36
2
annalesha's😈 Collection1💜 :
jaman c muanzie Manyon mbona mnatutesa
2026-08-29 14:52:18
3
Mwarabu :
mbna hyo ni wa Gairo mkoa wa mororgor ndgu shabiby
2026-08-29 18:35:21
1
issa tz :
shatiko na shatiko nitofaut
2026-08-29 14:48:19
0
Amiri Mnkombe :
mbona kama ni ndugu na shabibi?
2026-08-29 19:20:20
0
joany :
kwa hiyo SATCO hazitakuwepo Tena?
2026-08-29 15:38:24
0
Shaibu Hamisi :
🙏 ametusikiliza kilio chetu wana singida nashukuru sana 🥰🥰🥰
2026-08-29 20:51:26
1
user44755607875137 :
toweninajira
2026-08-29 12:37:20
0
wamigombani jr :
leta musoma to dar
2026-08-29 07:49:27
2
Abdul sasha :
warombo tumefikia sasa sio ngasere tena na Shabiby🥰
2026-08-29 17:14:07
1
Kingdull$_47 :
Naomba ruti ya mahenge moro hakuna gari huku
2026-08-29 15:32:38
1
Tech Master 🛠 :
Hivi Rombo hua kuna ninibmagari mengi sana yanaenda iyo njia 🤔
2026-08-29 15:25:05
1
Shaibu Hamisi :
mm ntakusapoti sana 🥰🥰
2026-08-29 20:52:23
1
sweet mangi👑 :
karibu sana 🫵
2026-08-30 07:48:08
0
ridax🇯🇲🍀☘️safi🍀 :
namba kaz
2026-08-30 10:40:24
0
To see more videos from user @ngasatvdodoma, please go to the Tikwm
homepage.