@infinitynest: Usidanganyike na mtu anayekuambia kifaa kinafika umbali wa kilometa fulani bila kukuuliza mazingira ya eneo lako. Umbali wa vifaa vya network hauamuliwi na nguvu ya kifaa pekee. Kuna vitu kama majengo, miti, milima, interference, line of sight na mazingira kwa ujumla. Kifaa kinaweza kufika meter 300 sehemu moja lakini sehemu nyingine kikashindwa hata meter 100. Kabla hujanunua kifaa, hakikisha umefanyiwa tathmini ya mazingira yako sio kuuziwa tu “hiki kinafika meter 300” 😅