@popmedia30: #HABARI:TAHARUKI imeibuka katika Shule ya Msingi Makota, Kata ya Masaka, Wilaya ya Iringa Vijijini, baada ya wanafunzi 13 wa Darasa la Saba kudaiwa kupigwa wakati wa maandalizi ya mtihani, huku baadhi yao wakifikishwa kituo cha afya kwa matıbabu. Tukio hilo limeibua mvutano kati ya wazazi na uongozi wa shule, huku wazazi wakidai watoto wao walichapwa kwa waya baada ya kushindwa kutoa Sh1,500 iliyokuwa ikikusanywa kila mwezi kwa ajili ya kuwalipa walimu wawili wa kujitolea. Hata hivyo, uongozi wa shule na mwalimu aliyetajwa katika tuhuma hizo wamekanusha madai hayo, wakisema wanafunzi walipewa adhabu kwa fimbo baada ya kukutwa wakicheza nje wakati wa muda wa kujisomea. Kwa mujibu wa wazazi na viongozi wa kijiji, tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili usiku wakati wanafunzi hao wakiwa wameweka kambi shuleni kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa Darasa la Saba unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao. Wazazi walidai baadhi ya wanafunzi walichapwa sehemu mbalimbali za miili, ikiwemo miguu, mapaja na mgongoni, huku wengine wakipata maumivu na kushindwa kutembea vizuri. #Iringaleo #WanafunziIringaleo #Walimuwakujitolea #Popmedia30
POPMEDIA
Region: TZ
Monday 31 August 2026 16:01:37 GMT
Music
Download
Comments
Mar Graphics Mar :
kwanini hamtaki kulipa ela za watu ,,lipeni mnapenda vya bure
2026-08-31 20:25:00
7
janie :
sas 1500 jmn mzazi nayo ni tatizo ah wazazi wengine wamezi
2026-09-02 10:48:57
2
Salu Juma :
walimu wakujitolea nishida
2026-09-01 20:14:35
2
seif Madole :
kwani Kuna sheria gani ya kupiga watoto
2026-09-01 01:09:25
1
Fidelis Tulashashe :
hii tabia sipendi walim kuwa chapa wanafunzi wakati watoto hawahusiki na utafutaji wa hela
2026-09-02 16:28:19
1
savio kp :
iyo shul naijua tulienda kufanya mtihan wa ujilani mwema mwka 2020😂😂😂😂
2026-09-01 15:12:54
1
loycenicolao119 :
jamani hivi walimu hawasikii jamani.....
2026-09-02 13:35:28
1
shemu :
wanadai haki zao
2026-09-02 13:33:46
1
FEBI AMBONISYE :
ila walimu
2026-09-02 09:56:20
1
kp🇰🇪 :
bwana mm nimecheka 😂😂😂😂😂😂
2026-09-02 12:44:22
0
Imani Amoni :
hao walimu ingekuwa vizuli wachukuliwe HATUA za kisheria hauuwezi ukampiga mwanafunzi kwasababu ya kuto kuja na ela zingatia Kwanza hao ni watoto hawana sehemu wanapo Fanya biashala kwajili ya kujipatia kipato na. kumpiga mtoto kwasababu hajaja na ela ni kumfundisha kwa kumfosi akaibe huo ni ujinga
2026-09-01 10:17:33
1
JitaMan :
duh
2026-09-02 14:08:40
1
R50 :
suala la walimu na michango ni sawa na traffic barabarani na rushwa kumbuka wote wapo serikalini
2026-09-01 07:49:48
1
user7110023581114 :
Kwa nn wasi itwe wazazi wanafunzi wanachapwa viboko kwa kosa ambalo sio lao hii sababu ya uongozi mbovu wa nchi
2026-09-02 14:52:33
1
m4 :
nyie walim kwanini mnaajili watu halafu pesa za kuwalipa mnategemea kwa wanafunzi hii ni ajabu aise
2026-09-02 03:43:48
2
Daniel Reuben :
Tanzania tutafika tumechoka sana, wazazi changieni watoto tupunguze maneno
2026-09-02 10:27:41
1
KIPINGI JR ⛪ :
sisi tulisha pigwa sana mbka hatutaman hata masomo tena yan kule hakuna selikali toka.zaman ya 😂😂😂
2026-09-01 19:35:35
1
loycenicolao119 :
aiseeee......Huzuni sana.
2026-09-02 13:36:00
1
Aggyie :
walimu wana szress
2026-09-01 16:31:21
1
mbogorechinord :
kwann mwalimu mchape mwanafunzi kwa kosa la mzazi ajaja na ela mrudishe nyumbani kwann mpiga
2026-08-31 21:16:24
1
Denis wa laizer :
Hao walimu wachukuliwe hatua Kali za kisheria
2026-09-01 12:40:15
1
V :
kuhusu hli swala me nlikuwa nkipingwa lakn sikutia ata mia adi nahitimu shule so Kwa makusudi but somo la hlo ambalo ni mathematics nlikuwa sielewi Moja Wala mbil
2026-09-02 18:36:43
1
Nafsa Hamis :
sas wanafunz ndo wanalipa au mzaz kakosa jmn
2026-09-02 14:16:23
1
fuadabdallah26 :
afungwe
2026-09-02 15:54:42
0
Mwajabu Alfani :
walimu ehee hii tena imexidi
2026-09-01 15:07:56
0
To see more videos from user @popmedia30, please go to the Tikwm
homepage.