@jambotv_: VIDEO: Baada ya mapumziko mafupi mchana wa leo, kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Antiphas Lissu, ilirejea huku Katibu Mkuu wa chama hicho, John John Mnyika, akipanda kizimbani kukabiliana na maswali ya dodoso kutoka kwa Wakili wa Serikali Mkuu, Nassor Katuga. Moja ya maeneo yaliyozua mjadala ni pale Katuga alipohoji kama raia yeyote, ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA, ana haki ya kuzuia uchaguzi mkuu uliowekwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi. Mnyika alitoa jibu akisema, "Ni haki kwa uchaguzi usio huru na wa haki, ni haki kuuzuia kwa njia za kidemokrasia. Ni haki kabisa". Amesisitiza kuwa wananchi wana haki ya kushiriki uchaguzi ukiwa huru, wa haki na halali tu. Katuga alimtaka Mnyika kufafanua kile alichokisikia wakati wa hotuba ya Tundu Lissu katika mkutano wa watia nia wa Aprili 3, 2025. Mnyika alikiri kusikia kauli za ‘Polisi kukimbia na mabegi ya kura’, ‘tunaenda kuzuia uchaguzi’ na ‘tunaenda kukinukisha’ akisema kuwa Lissu alifafanua kauli hizo. Katuga alipohoji kama Mnyika ameleta mahakamani hotuba hiyo inayofafanua maneno hayo, Mnyika alijibu: "Nimeileta kwa maelezo ya mdomo kwasababu si wajibu wangu kuthibitisha mashtaka". Katuga alijaribu kumjenga Mnyika kama shahidi mwenye masilahi binafsi (interested witness) katika kesi hiyo, kwa kuwa uteuzi wake kama Katibu Mkuu ulipendekezwa na mshitakiwa (Tundu Lissu), na kwamba yeye ndiye aliyeratibu kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 29 Agosti 2026 kilichoazimia kumtetea Lissu kwa nguvu zote. Mnyika alikataa vikali madai hayo akieleza kuwa masilahi yake katika kesi hiyo yanawakilisha masilahi ya chama (party interest) na masilahi ya umma (public interest), na siyo masilahi yake binafsi.
Jambo TV
Region: EN
Monday 31 August 2026 18:44:36 GMT
Music
Download
Comments
c'est Le Fraitel :
very clean response
2026-09-01 17:30:33
0
Simon :
mungu simamia kesi ya lissu
2026-08-31 23:52:27
6
My1 :
Mstakiwa ni Mwansheria, shahidi ni mwanasheria. kazi kweli kweli
2026-09-01 13:44:10
0
pattiepatrice :
masilahii kwnn mtahabixhe mwenzenu hvo
2026-09-01 13:34:11
0
user18341719390250 :
chadema wote ni wanashelia
2026-09-01 12:44:01
1
furaha :
Mungu simama na mashahidi wa Lisu
2026-09-01 14:30:28
0
Freeman :
2026-09-01 14:35:47
0
PELEGORE 🤔🤔🤔🤔 :
Nakubali
2026-09-01 17:52:46
0
Dorcas :
2026-09-01 09:38:02
0
kamwana :
Nawaombeeni wa Tanzania mpate katiba mpya itakayo tambua haki za wa' Tanzania. Mungu mbele ndugu zetu waTanzania🫶
2026-09-01 12:33:21
0
user53420233585950 :
Pamoja Mungu awstetee
2026-08-31 20:33:34
1
mpenda haki :
Amina mnyika
2026-08-31 20:17:38
0
Eng Senator :
Mungu atasimama pamoja nanyi
2026-09-01 04:33:50
0
Abdallah Kibeku :
chizzzz
2026-09-01 19:11:47
0
Katemi :
tutashinda kwa kishindo, dhuruma ina mwisho wake
2026-09-01 10:44:34
0
Masunzu Furniture :
nikweli mnyika hana masilahi na lisu
2026-09-01 04:35:56
0
user47266941046922 :
Raha ya viongozi wa chadema ni vichwa kweli kweli. Ushindi kwao ni mkubwa! Mungu yu pamoja nanyi.
2026-09-01 15:08:35
0
Kain Mtuluwa :
kumbe munyika nae Yuko vizuli sana
2026-09-01 20:16:38
0
George Njaro Mollel :
😁😁😁
2026-08-31 19:47:50
0
Bahati Windo :
💪💪💪
2026-08-31 21:06:16
0
Bill :
😳😳😳
2026-09-01 19:25:07
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm
homepage.