@the3amaltar: *NOVENA YA MT FILOMENA.🛐🙏* *(SALI SIKU 9 NOVENA HII.)* *SIKU YA KWANZA.* 🛐🛐🛐🛐🛐🛐 Ee bikira mwaminifu na mfia dini mwangavu na mtukufu, unayetenda miujiza mingi nayapekee. Kwaajili ya masikini na wanaoteswa, unihurumie na mimi pia. Wewe unajua wingi wa matatizo yangu na mahitaji yangu. Tazama, nimejitupa chini miguni pako. Nimejaa uchungu, lakini pia ninamatumaini tele. Ninausihi wema na Upendo wako, Ee mtakatifu mkubwa. Tafadhali unisikilize kwa wema na unipendekeze kwa Mungu ili anikubalie kwa huruma na kunijalia fadhili hii ninayoiweka mbele yako. *(Taja/sema hitaji lako...........)* Nina hakika dharau, mateso na kifo ulivyo pitia, kwa kuyaunganisha hayo yote na mastahili ya mateso na kifo cha Yesu mchumba wako wa kimbingu, nitajaliwa fadhili hii niliyokuomba. Na kwafuraha ya Moyo wangu, nikimtukuza Mungu aliye mstaajabivu katika watakatifu wake. 🛐 Amina🛐 ♦️♦️♦️♦️♦️♦️ *Litania ya Mtakatifu FLOMENA.* ➕ Bwana utuhurumie... Bwana utuhurumie ➕ Kristo utuhurumie... Kristo utuhurumie ➕ Bwana utuhurumie... Bwana utuhurumie ➕ Kristo utusikie... Kristo utusikilize 🛐 Baba wa mbinguni, Mungu.. (Utuhurumie) 🛐 Mwana Mkombozi wa dunia Mungu (utuhurumie) 🛐 Roho Mtakatifu Mungu (utuhurumie) 🛐 Utatu Mtakatifu Mungu (utuhurumie) *♦️ Kiitikio UTUOMBEE* ➡️ Maria Mtakatifu malkia wa mabikira ➡️ Mtakatifu Flomena uliyejazwe neema nyingi tangu kuzaliwa kwako ➡️ Mtakatifu Flomena mfuasi mwaminifu wa Maria ➡️ Mtakatifu Flomena kielelezo cha mabikira ➡️ Mtakatifu Flomena hekalu la unyenyekevu Amini ➡️ Mtakatifu Flomena mwenye bidii na utukufu wa Mungu ➡️ Mtakatifu Flomena uliyeteswa mintarafu mapendo ya Yesu ➡️ Mtakatifu Flomena mfano wa nguvu ya kudumu katika Sala ➡️ Mtakatifu Flomena usiyeshindwa kwa usafi wa Moyo ➡️ Mtakatifu Flomena kioo cha matendo ya kishujaa ➡️ Mtakatifu Flomena imara na usiyetishika mbele ya mateso ➡️ Mtakatifu Flomena ukiyepigwa mijeledi kama mchumba wako wa mbingu ➡️ Mtakatifu Flomena uliyepigwa mishale mfululizo ➡️ Mtakatifu Flomena uliyefarijiwa na mama wa Mungu ukiwa umefungwa minyororo ➡️ Mtakatifu Flomena uliyeponywa kimiujiza gerezani ➡️ Mtakatifu Flomena uliyefarijiwa na Malaika katika mateso ➡️ Mtakatifu Flomena uliyechagua mateso ya kifo kuliko fahari ya kiti cha ufalme ➡️ Mtakatifu Flomena uliyewaongoa walioshuhudia kifo chako ➡️ Mtakatifu Flomena uliyeshinda hasira za watesi wako ➡️ Mtakatifu Flomena mlinzi wa wasio na kosa ➡️ Mtakatifu Flomena msimamizi wa vijana ➡️ Mtakatifu Flomena kimbilio la masikini ➡️ Mtakatifu Flomena afya ya wagonjwa na wanyonge ➡️ Mtakatifu Flomena unayeangamiza upagani wa ulimwengu ➡️ Mtakatifu Flomena unayeamsha Imani na nguvu za waamini ➡️ Mtakatifu Flomena ambaye jina lako limetukuzwa Mbinguni na kuogopwa kuzimuni ➡️ Mtakatifu Flomena uliyefanywa maarufu mintarafu muujiza ya ajabu ➡️ Mtakatifu Flomena mwenye nguvu kwa Mungu ➡️ Mtakatifu Flomena unayetawala katika utukufu 🔵 Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za ulimwengu... *Uturehemu ee Bwana* 🔵 Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za ulimwengu... *Utusikilize ee Bwana* 🔵 Mwana kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za ulimwengu... *Utuhurumie* *(K)* Utuombee Mtakatifu mkuu Flomena *(W)* Tujalie ahadi za Kristo _*TUOMBE*_ Tunakusihi ee Bwana kwa maombezi ya Mtakatifu Flomena, Bikira wa shahidi aliyependeza machoni pako daima kwa njia ya utakatifu wake mkuu na fadhila ya uadilifu, Utusamehe makosa yetu na utujalie neema tunazo hitaji *( ongeza ombi lolote hapa....)* *Amina*🛐🙏 #tanzaniantiktok🇹🇿 #tanzaniantiktok🇹🇿 #tanzaniantiktok🇹🇿 #kenyantiktok🇰🇪 #kenyantiktok🇰🇪

THE 3AM  ALTAR 2026
THE 3AM ALTAR 2026
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 01 September 2026 05:34:06 GMT
535
52
4
8

Music

Download

Comments

gloryromeo6
gloryromeo6 :
Amina
2026-09-01 06:28:48
0
saimon.tadei
Saimon Tadei :
Amen
2026-09-01 06:43:08
0
victoriakilangi
victoriakilangi :
Amina
2026-09-01 06:42:52
0
princessnoratee
princessnoratee :
🙏🙏🙏
2026-09-01 06:51:43
0
To see more videos from user @the3amaltar, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About