@eternalinternationalhq: 🥛 Baadhi ya watu wakinywa maziwa, tumbo linaanza kufanya vurugu! 😂 Gesi, tumbo kujaa, kuunguruma, maumivu ya tumbo au kuharisha baada ya kutumia maziwa vinaweza kuwa dalili za Lactose Intolerance. Hii hutokea pale mwili unapokuwa hautengenezi kimeng'enya cha kutosha kinachoitwa lactase, ambacho husaidia kumeng'enya lactose—sukari inayopatikana kwenye maziwa. Lakini kumbuka, lactose intolerance siyo sawa na allergy ya maziwa. 👉 Wewe ukinywa maziwa, tumbo lako huwa sawa au linaanza kufanya vurugu? Tuambie kwenye comments. #InsideYourBody #LactoseIntolerance #Afya #AfyaYaTumbo #EternalInternational