@sebastiangabuliery: #UPDATES_KESI_YA_UHAINI_YA_TUNDU_LISSU #Leo_Jumanne September 01,2026 #Sehemu_ya_375 👉WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN MNYIKA MAHAKAMANI Nassoro Katuga: Mtandao wa Jambo TV ni nini? Mnyika: Online TV ya Jambo TV. Nassoro Katuga: Nitakuwa sahihi kwamba kuna mtandao unaitwa Jambo TV? Mnyika: Sifahamu. Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa, ushahidi huu uliotoa siyo ushahidi wako, ni ushahidi wa kuambiwa. Mnyika: Ushahidi upi sasa? Nassoro Katuga: Ulisema uliambiwa kwamba maneno yamechapishwa Jambo TV. Mnyika: Sahihi. Nassoro Katuga: Kwa hiyo, swala la kuchapisha haya maneno siyo ushahidi wako, bali ni ushahidi wa kuambiwa? Mnyika: Ni sahihi. Nassoro Katuga: Ni majibu yako kwamba mkutano wa tarehe 03 Aprili 2025 haukuwa na Mwenyekiti? Mnyika: Ni majibu yangu. Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kwamba mikutano ya CHADEMA haina Mwenyekiti. Mnyika: Siyo mikutano yote haina Mwenyekiti. Nassoro Katuga: Waambie Majaji kwamba chama chetu mikutano haina Mwenyekiti. Mnyika: Inategemea na aina ya mikutano. Nassoro Katuga: Waambie Majaji kwamba mikutano haina muhtasari (minutes). Mnyika: Haina muhtasari. Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama mikutano ya CHADEMA isiyokuwa na Mwenyekiti ina ajenda. Mnyika: Inaweza kuwa na ajenda au isiwe nayo, inategemea na aina ya mikutano. Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama mkutano wa tarehe 03 Aprili ulikuwa na ajenda. Mnyika: Haukuwa na ajenda, ulikuwa na mada. Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, mada inamaanisha nini na unatofautisha nini na ajenda? Mnyika: Kwa mujibu wa Katiba... Nassoro Katuga: Ujue nina... Lissu: Waheshimiwa Majaji, shahidi anaulizwa swali kabla hajajibu anazuiliwa kujibu. Huu ni utaratibu gani? Nassoro Katuga: Kwanza sijajua ni objection au ni kitu gani. Lissu: Ni objection. Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, nijibu objection. Jaji Ndunguru: Endelea na cross-examination. Nassoro Katuga: Ukisema mkutano wa tarehe 03 Aprili haukuwa na ajenda? Mnyika: Haukuwa na ajenda, ulikuwa na mada. Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama huo ulikuwa mkutano wa kichama au wa mafunzo. Mnyika: Mkutano wa kichama wa kueleza na kusikiliza mawazo. Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji utofauti wa mada na ajenda. Nassoro: Natumia maneno ya Kiingereza, mada ni topic. Naamini Waheshimiwa Majaji watakuwa wameelewa, mada ni topic. Nassoro Katuga anaenda kwa wenzake kuteta, kisha anarudi tena. Nassoro Katuga: Hiyo tafsiri ya mada na ajenda ni ya kwako au kwa mujibu wa kamusi? Mnyika: Kwa tafsiri yangu. Nassoro Katuga: Naomba, kwa ridhaa ya Mahakama, nimpe kamusi. Mnyika: Hii nini? Nassoro Katuga: Kamusi Kuu ya Kiswahili ya BAKITA. Nassoro Katuga: Soma hapa. (Anamuonyesha.) Mnyika: Ajenda ni orodha ya mada itakayojadiliwa katika mkutano; mambo ya kujadiliwa katika mkutano. Nassoro Katuga: Kwa tafsiri ya hapa kuna tofauti kati ya mada na ajenda? Mnyika: Naomba nipewe kamusi nisome mada pia kwa tafsiri yake. Mnyika: Mada ni jambo linalojadiliwa. Nassoro Katuga: Je, kuna tofauti ya mada na ajenda? Mnyika: Ni vitu viwili tofauti. Ndiyo maana kamusi imeweka maneno tofauti. Isingekuwa tofauti, kungekuwa na neno moja. Nassoro Katuga: Kwa tafsiri hii bado unataka kusema kwamba mkutano wa tarehe 03 Aprili haukuwa na ajenda? Mnyika: Ni sahihi, hapakuwa na ajenda; palikuwa na mada. #MrbugaluNews #followmrbugalu
@MrBUGARU
Region: TZ
Tuesday 01 September 2026 08:03:41 GMT
Music
Download
Comments
lucky :
Agenda ni mtiririko Wa mambo ambayo yanaenda kufanyika katika mkutano
mada ni jambo mahususi au maalum lilichaguliwa ili lifanyiwe mazungumzo, mdahalo
2026-09-01 16:08:31
9
Victoria GL :
washabananishwa
2026-09-08 04:54:50
2
halima alhaj :
mada ni topic ahende ni kama instruction
2026-09-01 19:57:56
1
Msami Shemu :
wamezoea majukwaan kutukana hamna kitu yyte wanajua hao mpk mahakaman wanataman kutusi ila ndo hvo hawajiwezi mbele ya Sheria
2026-09-18 03:29:33
0
""The Matthew Jr"" :
Mahakama siyo jukwaa la kisiasa....!!
2026-09-05 17:20:46
0
Makala@tz :
Endeleeni kubishana kisiasa acha sheria inene
2026-09-01 10:02:37
0
halima alhaj :
mada na ajenda ni vitu vuwili tofauti kwel mnyikaa fud
2026-09-01 19:57:22
0
kilutile :
huwezi kwenda kwenye mada bila kupita kwenye ajenda mnyika bado sana sijui ukatibu alipataje
2026-09-01 08:23:17
4
canjani owen :
wengi wapo kwenye ushabiki huyu katunga balaa njingine la mjini
2026-09-05 23:05:38
0
To see more videos from user @sebastiangabuliery, please go to the Tikwm
homepage.