@nuktatanzania: Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi, amehoji hatua zinazochukuliwa na Serikali kuhakikisha taaluma ya udereva inapata hadhi, stahiki na heshima kama zilivyo taaluma nyingine. Swali hilo limejibiwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Regina Qwaray, leo Septemba 1, 2026, Bungeni jijini Dodoma. Aidha, jambo hilo lilimfanya pia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo, kuingilia kati na kusema kuwa sekta ya usafirishaji ni muhimu katika uchumi wa taifa, huku madereva wakiwa ndio wanaoiendesha sekta hiyo. Alisema madereva ni watu muhimu katika sekta hiyo, hivyo Serikali itaweka mkazo katika kuhakikisha wanaendelea kuheshimiwa nchini.
NuktaTanzania
Region: TZ
Tuesday 01 September 2026 09:04:21 GMT
Music
Download
Comments
amir mariale :
inauma mno mikataba hakuna mafuta hayatoshi
ukija barabaran fain ni nyingi
2026-09-02 12:16:02
2
Stanley Silvanus :
wahongo selikari haina mpango wowote na madereva hasa wale madereva wa makampuni binafsi wanapewa mikataba feki hakuna likizo mishahara hawapat wanaish kwa posho tu yan gari likipak hapati malipo yeyote
2026-09-01 19:16:14
3
GodfreyTowo :
pia upatikanaji wa leseni umekua shida sana
2026-09-02 07:53:15
0
pharyhwaph :
madereva wa mashule wananyanyasika
2026-09-02 07:04:35
1
HEHE BOE 💵 driver 🛣️🚛 :
huo ni uongo mtupu
2026-09-02 20:56:53
0
omar khan :
huwa yanaishiaga huko huko
2026-09-02 19:07:39
0
Athumani Madomba :
serikali ipo sawa ila wale wanao simamia ndyo kipengele utendaji sio sawa
2026-09-02 11:03:19
1
Pesambili :
Kiukweli sisi maderva tunakua kama mabaamerd tu selikali haitujali kabisa tunazauliwa na hatupewi malipo yetu yanayostahili, kiukweli serikali tunaomba mliingilie kati hiliswala
2026-09-02 09:38:35
0
Magulu Nnyondo :
zungumzieni pia wawe na bima ..
2026-09-02 21:10:54
0
SEVEN DASH🇹🇿✊🏿 :
yangu macho
2026-09-02 04:52:55
1
lugano,yanga sport :
katika kitu hatuwamiini ni nyie jamaa
2026-09-03 00:29:51
0
msaka shiling :
kama kweli serekali inaona umuhimu wa madeva tonaomba serekali itenge muda wakupitia kila mkoa na kila campan naami itagundua mambo mengi sana
2026-09-01 09:15:29
2
econwoo :
ni uongo
2026-09-02 14:09:20
0
Moses Misalaba :
madereva wanateseka sana shida sana mateso tu Kwa madereva
2026-09-02 17:54:35
0
Ahmed msambara :
mnawafata matajiri nyie viongoz mnachukua rushwa ili madereva wanyanyasike
2026-09-01 20:49:33
1
Hans 07 :
Hawa watu sijui walichaguliwa na nani
2026-09-01 10:48:21
0
peterkulwa982 :
mm nimesikiliza ila sijaelewa alie elewa anieleweshe
2026-09-01 13:44:26
1
Magulu Nnyondo :
tengenezeni barabara ziwe nzuri ajari nyingi ..mafoleni mlandizi mpaka morogoro
2026-09-02 21:09:36
0
Ngella :
hizi siasa zenu kwenye senta ya uderva ipo sk itafka mwisho na tutapewa heshim yetu na mchango wetu mkubwa tulio utoa ktk nchi yetu ya tanganyika lkn sio kwa utawala wa ccm ndio kwanza mumefnya maisha yetu yawe mangumu zaid kuliko hata huko tuliko toka
2026-09-02 12:13:02
0
user6093786125559 :
mnatudanganya
2026-09-02 13:05:19
0
Dominic Emmanuel :
hata selekali inatubana
2026-09-02 12:57:47
0
kassim thabit :
Asante mheshimiwa mungu akujalie kwa kutusemea kwakweli ni shidaa
2026-09-03 09:26:24
0
Baba J D :
hakuna dereva daladala mwenye mkataba kama kweli mko siliasi ingenious barabarani simamisheni kila daladala mwambie dereva akupe mkataba
2026-09-02 14:48:12
0
Sheby lv :
tumekubari kusoma sasa nanyie mtuzingatie
2026-09-02 15:49:22
0
mawigi :
rashidi alikuwa meneja wangu uyuu kwenye lor pambana bbu
2026-09-01 12:22:38
0
To see more videos from user @nuktatanzania, please go to the Tikwm
homepage.