@chawamata_tv: VIDEO: Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Mohamed Salum, amesema matumizi ya reli pekee hayawezi kwa sasa kumaliza changamoto ya usafirishaji wa makontena kutoka Bandari ya Dar es Salaam kutokana na uwezo mdogo wa reli kubeba mizigo. Akizungumza kuhusu mpango wa kutumia reli kusafirisha makontena kwenda Kwala, Salum amesema treni moja kwa sasa ina uwezo wa kubeba takribani makontena 27 kwa safari moja, hali ambayo haiwezi kukidhi mahitaji makubwa ya bandari yenye kiwango kikubwa cha mizigo. Amesema hata kama treni ingeweza kufanya safari nyingi kwa siku, bado kungekuwa na pengo kubwa kati ya uwezo wa reli na kiwango cha makontena yanayoingia na kutoka bandarini, hivyo matumizi ya malori hayawezi kuondolewa kwa sasa. “Kwa uzoefu wangu, sijawahi kutembea bandari duniani ambayo haina malori. Kama kuna mtu ataje bandari moja inayofanya huduma za makontena bila malori,” amesema Salum. Amesema malori ni sehemu muhimu ya mfumo wa usafirishaji wa mizigo kwa sababu yanarahisisha uhamishaji wa makontena kutoka eneo moja kwenda jingine, hususan pale ambapo uwezo wa reli bado haujakidhi mahitaji. Salum amesema wakati Serikali ikiendelea kuboresha reli ya SGR, bado kuna umuhimu wa kutumia njia zote mbili za usafirishaji, yaani reli na barabara, ili kuhakikisha shughuli za bandari zinaendelea bila kusababisha msongamano wa mizigo. Ameeleza kuwa bandari inapopokea makontena kutoka kwenye meli, wakati huohuo kuna makontena ya kusafirisha nje ya nchi yanayopaswa kuingizwa bandarini, pamoja na makontena matupu yanayohitaji kuingia na kutoka. “Shughuli ya bandari siku zote inategemea logistics kubwa ya reli na barabara,” amesema Salum. #ChawamataTV #10KFollowers #Asanteni #DarEsSalaam #Tanzania #Bongo #Habari #HabariLeo #BreakingNewsTZ #TanzaniaNews #bongoupdates#mediatanzania #tanzaniatrendingvideos #tanzaniatrending #tanzaniatrendingstory #TanzaniaTre #madeintanzania🇹🇿 #madeintanzan #madeintanzania #SupportLocal #madeintanzaniat #roadto100followersontwitch #madeintanzaniawith #viraltz
CHAWAMATA TV
Region: TZ
Tuesday 01 September 2026 09:43:12 GMT
Music
Download
Comments
jmarick5 :
ukiweka ugumu moyoni hata kuchwa kinakuwa kigumu
2026-09-01 10:47:43
20
Babu T :
huyu jamaa kaongea fact sana
2026-09-01 10:41:26
4
mtaalam :
kwanin hayo malori yasipeleke kwala?
2026-09-01 14:11:48
2
mapene :
chawamata zambia 🇿🇲 trafik wanasumbua sana yani isoka na chinsali na mbala wameshaanza mnatusaidiaje
2026-09-01 12:17:36
2
user7782346947487 :
Daah kuna maswali mengi sana hapo kwenye maelezo yke ambayo hawez kuyajibu wakati Unafanya upanuzi wa bandari lazima iendane na upanuzi wa miundo mbinu mingine ukiongeza uwezo wa bandari ukaacha vitu vingine Vya msingi lazima ufeli tuu
2026-09-01 11:31:20
10
kesatz :
Awa ndo wanaokula mema ya nchi .. ndo waajiriwa wenyewe
2026-09-02 10:15:54
2
dar.car.service :
Wana park hadi kwenye njia za dharura, mageti ya nyumba za watu, issue ni kufuata utaratibu na sio kuzuia njia zote mbona tangu RC ameelekeza barabara hazina foleni ya kupitiliza kama awali, pia yafanyiwe service yasifie barabarani na kuwe na uondoaji wa haraka linapokuwa limeharibika
2026-09-01 12:55:59
2
mnyanda :
treni inabeba kontena 27 kwanini musinunue mabehewa yakobebea izo kontena,
2026-09-01 14:08:02
2
LIFE IS ART :
mtazamo wangu hapa kuna mkwamo mkubwa wa kifra na maamuzi mazito. yani sgr imejengwa treni zimemunuliwa. imeshindikanaje kununua treni na mabehewa hata 1000. ruti 2-3 kwasiku. huku ni kuendekeza shida.
2026-09-01 12:18:36
7
simple but heavy :
tatizo maeneo mengi wataalamu kama hawa wanapuuzwa siasa inachukuwa nafasi
2026-09-02 12:48:37
0
Barageti_10🇹🇿 :
huyu jamaa ukimsikiliza ukiwa umelegeza fuvu utamwelewa..
kwel meli ikiwa inashusha huwa inapakia na meli inaenda na muda. itafika kipind tukubal makaz kupisha bandar tuu tuje kuishi kibaha
2026-09-01 11:47:12
2
swalehebori495 :
toa ICD zote mjini
2026-09-01 17:39:44
1
Denisdamian :
hii serikali yani unapanua bandari unafanya ukarabati wa bandari lakini hayo malori ya kupakia na kushisha mnashindwa kuyatenhenezea miundombinu, yani mnashindwa kutanua Barabara mnategemea nini?? Lori na magari yakwaida yanakaa Barabara moja Tena yamebeba Tani za kutosha hii ni hatari 😢
2026-09-01 17:30:24
2
moudykisengo :
sawa ,,,kwann mnatoa vibali vya icd adi mitaan bila kuangalia maisha ya watu ,,kwan msiwaambie watu wakajenge icd pembezon mwa mji wa dar
2026-09-01 11:22:34
1
idrissamohamed16 :
Njooni Mtupe Hela Njema Tugawane Urithi Mkubwa 🤣🤣🤣
2026-09-10 04:40:37
0
Chao :
kwaiyo kwala imejengwa kimakosa?
2026-09-04 04:48:50
0
user9057020538816 :
wanao elewa Maswala ya bandari mana yake nini ndo hao , sio wengine wanabwabwaja tu .
2026-09-01 10:15:56
3
duddywily :
kwahyo unamsema chalamila au?
2026-09-01 12:19:12
0
Nizar Khan850 :
So kuweka icd mjini na sehemu wa makazi Sawa. Kwanini msipeleke nje ya mji. Iyo sio solution.
2026-09-17 19:41:52
0
osman :
hujaongeakitu kabisa
2026-09-03 18:50:07
0
Brazilero :
hawa ndio watanzania
2026-09-05 16:37:42
0
mikidad mussa :
sisa na kazi havichangaman
2026-09-04 04:22:30
0
solar_iq_tz :
PUNGUZENI KODI HILI WATU WAPATE MIZIGO YAO KWA ULAHISII MIZIGO INAKA SANA KWASBABU WENGI WANASHINDWA KUTOWA KWA WAKATI KWASABABU MALINDIKO YA KODI NA MADENI.HILA KODI ZIKISHUKA WATU WANAWEZA KUTOWA MIZIGO KWA HALAKA KWASABABU GHALAMA INAKUWA NDOGO NA ANAWEZA FATILIA KWA WEPESI KWASBABU HATUMII GHALAMA KUBWAAA
2026-09-03 20:22:34
0
Denice Burchard :
Kwann msijenge barabara maalumu kwa ajili ya malori
2026-09-10 12:31:01
0
Theki84 :
Kwa kifupi tulikosea itabidi ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uwe wa kasi hapa Dar es salaam tulishakosea anachoeleza hapo dah
2026-09-01 12:23:53
0
To see more videos from user @chawamata_tv, please go to the Tikwm
homepage.