@openonlinemedia: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amesema Serikali itaendelea kuweka mkazo katika kuboresha mazingira ya kazi na kulinda heshima na haki za madereva nchini, akisisitiza kuwa kundi hilo ni nguzo muhimu katika sekta ya usafiri na usafirishaji. Prof. Mkumbo ameyasema hayo leo Septemba Mosi, 2026 Bungeni jijini Dodoma wakati akiongezea majibu ya Naibu Waziri kuhusu hoja ya Mbunge wa Mlalo, Mhe. Rashid Abdallah Shangazi, iliyohusu changamoto mbalimbali zinazowakabili madereva nchini. Amesema sekta ya usafiri na usafirishaji ni miongoni mwa sekta muhimu zinazochochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania, ikichangia asilimia 8.5 ya uchumi na kutoa ajira kwa takribani asilimia 4.4 ya nguvu kazi nchini. Kwa mujibu wa Prof. Mkumbo, Tanzania inakadiriwa kuwa na madereva kati ya milioni 1.1 hadi 1.3, idadi inayoonesha kwa kiasi kikubwa nafasi yao katika kuendesha shughuli za kiuchumi na kijamii. Amesema kupitia Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Serikali imelenga kuongeza ajira zenye staha na hivyo itaendelea kutoa kipaumbele kwa sekta hiyo, ikiwemo kuhakikisha madereva wanapata mazingira bora ya kutekeleza majukumu yao. Aidha, Prof. Mkumbo ameshauri kuwa endapo kutabainika vitendo vya dhuluma, uonevu au ukiukwaji wa haki dhidi ya madereva, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inapaswa kufuatilia changamoto hizo na kuhakikisha haki za madereva zinalindwa. Amesisitiza kuwa uboreshaji wa mazingira ya kazi kwa madereva ni sehemu muhimu ya kujenga sekta ya usafiri na usafirishaji yenye tija, inayoheshimu utu na inayochangia kikamilifu maendeleo ya taifa. #Pakua App ya #OpenMedia playstore kusikiliza #DoubleORadio na kutazama #OpenMTV au kupitia tovuti #openmedia.co.tz, Kwa Matukio, Habari na Matangazo wasiliana nasi 0677107271 au 0677107273.
Open Online Media
Region: TZ
Tuesday 01 September 2026 09:52:11 GMT
Music
Download
Comments
@%.MALUNGA&&%🫡🫡 :
fact father
2026-09-10 05:05:13
0
MŪJĀHDŪN :
Jaman WENYE class D tunateseka uku kwenda class E,miaka mi3
2026-09-02 07:50:13
8
khalfan daud :
BUNGE MTUSAIDIE TUNATESEKA SANA NA SWALA KUKATA POINTS
2026-09-09 20:21:13
2
John David :
kiukwer tunahali ngumu sana madereva
2026-09-10 19:24:26
1
Shadrack Jofrey :
serekari mnatutesa.madereva yan hakuna namna yan
2026-09-01 19:24:14
4
Mr Lutufyo :
waifanye kasi ya udereva kuwa sekta rasmi,iwekewe taasis kama zilivo sekta zingine.
2026-09-10 10:28:55
2
9876543210 :
ila bado hakuna point
2026-09-01 14:49:56
1
Pasha Khamis :
hakuna haki secta hii dhulma imejaaa mimi nimedhulumiwa ila mungu atanisimamia ipo siku nitakutana na mtetezi wangu yuko hai
2026-09-02 04:05:10
1
Mdau :
Hilo swala nilakuwapumbaza madeleva HAKUNA KITUHAPO😡😡
2026-09-02 01:09:47
3
amir mariale :
tunaomba pia mtufutie na Sheria zingine barabaran hazina maana zaid ya udhulumaji
Moja ondoeni fain za fast aid kwakuwa hakuna pia sheria ya kumruhusu mtu kumilik dawa na hakuna Sheria ya mtu kunywa dawa bila kibali na je nani anakagua hizo dawa walizonazo kwenye fast aid
pili Kuna fain tunapiga kisa huna stika ya RHD Kwan askari akisimamisha gar haoni dereva yupo upande gani
2026-09-02 12:05:01
5
SEVEN DASH🇹🇿✊🏿 :
acheni kutu pumbaza bhn tunadhulumiwa sana na hamfanyi chochote
2026-09-02 04:43:21
2
yusuph rod :
ivi kwanini hawa polisi wanaleta kilasiku mbinu za kumkanda miza dereva wataishi vp pia wao kama huyu dereva ata amua kukaa nyumbani
2026-09-10 18:13:42
0
waziriitambu :
sikiliza wewe kiongozi kama nikweli unalosema kwann nyie mnalazimisha tukasome wakati watu wameendesha gari zaidi yamiaka 30 unamyambia akasomeenii mituibiepesa tunajua nyie viongoz wakisiasa niwaongo saaana nahamuaminiki kabisa kwasababu mnawaambia wtumishi wenu wawe wabunifu kuongeza mapato mapya hatuwapendi kabisa niomaana mkifa raia wanafurahia saaana mnajiona kawa tz yakwenu pekeyenu sisi raia haituhusu kabisa
2026-09-01 17:35:47
5
Seve Baba :
sio muishie kuongea tu mfanye utekerezaji tumechoshwa na maneno yenu pasipo utekerezaji.
2026-09-02 08:57:34
1
H.H.H.🇹🇿V8 :
bado hakuna point
2026-09-01 13:51:17
2
jackson :
sio apa bongo
2026-09-01 13:59:48
0
kz fainest :
mnatutesa sana jaman kama mnataka tuwe wez mtwambie
2026-09-10 06:53:53
5
Joseph :
Mnatunyanyasa sana dereva akiwa kazini kwake ni kama tuko vitani. polisi ,latra,
2026-09-02 04:02:13
1
Mathias Lyuma :
Kwa Africa ndo nchi pekee inayomuona dereva hana umuhimu angalia congo dereva analipwa dollar 600 adi 2000 kwa mwezi kwa kaz za migodi transit ndo wanalipwa vizuri zaidi njoo Tanzania sasa ata aibu hawaoni nafasi za kaz mshahara 400,000 jmn hiv huyu dereva ata kuvaa atavaa kweli serikali hiliangalie hili
2026-09-01 21:11:17
1
Omary Hayni :
nikweli muna 2tesa wenye familia kam 2na watot nafamilia zina 2angalia munataka mu2 weke maisha gani au muna taka wa2 wawe wez naomba liangalien ilo madeleva watawalani nafamilia zao embu weken msimamo laisi maana unaenda kusoma alafu mwengine ajui kusoma sema alama ana zijua kwalug yake yatazania ata shule kafeli mchong wapei ata pata pei wap akat hana kazi
2026-09-10 23:35:31
0
Finias Banele :
je na hiyo report ya mkuu wa police ya kukata points kaipata wapi
2026-09-10 20:26:50
0
munymwezi8 :
🙏🥰🥰🥰🥰🥰🥰🥰🥰🥰🥰🙏🙏 tumeaza kisikika sasa
2026-09-10 18:53:00
0
benjaminnzumbi :
hapo manyanhaso mengine tuliyakubali ila la pointi ni chanvamoto jmn
2026-09-10 17:18:08
0
JANJARO TRUCK DRIVER🇹🇿 :
madereva mnatutesa sana adi imefkia wakat tunaichukia nchi yetu
2026-09-10 21:11:17
0
omary omar kiria :
matari Wana tupa gari mbovu VP leseni za kwao mbona ni dereva wakati dereva hanuni tayiri walla usajili lakini ndio mna tubebesha
2026-09-10 21:19:27
0
To see more videos from user @openonlinemedia, please go to the Tikwm
homepage.