@masterjimmy_tz: Leo nimekutana na freestyle ya msanii maarufu kwa jina la Nyabingi. Jamaa ana uwezo mkubwa sana wa kurap na yupo local kweli. Kwenye moja ya mistari yake amesema kuwa haimuumizi sana kutokujulikana, muhimu kwake ni kuendelea kuchana. Hii imenifanya nijiulize: alikuwa anamaanisha nini? Je, ni kwamba kwake Hip Hop ni zaidi ya umaarufu na mafanikio ya kibiashara? Kuna wasanii wengi wa Hip Hop Bongo wenye uwezo mkubwa kwenye freestyle na cypher, lakini bado hawajapata nafasi kubwa ya kutoboa kwenye mainstream. Wengine wanaishia kusifiwa kwa kuwa “wakali” kwenye cypher, lakini wanapoweka kazi zao rasmi wanaonekana kutopata mafanikio makubwa. Mfano wa wasanii kama Cado kitengo, Boshoo Ninja, Wizzy MP na Toxc Fuvu. Swali kwa mashabiki wa Hip Hop Ni msanii gani mwingine unayemfahamu ambaye ni mkali sana kwenye freestyle, ana kipaji kikubwa, lakini bado anajitafuta kutoboa?
Jimson Natson
Region: TZ
Tuesday 01 September 2026 18:49:50 GMT
Music
Download
Comments
SIMBA OUTFIT 🔥 :
Ila Hii beat ni balaa lingine 🎶🎼
2026-09-09 12:55:39
2
yahayamnango :
Nyabingi unakinukisha kweli
2026-09-12 02:54:41
0
k.i.l.o-tz%sd :
kak unajua san
2026-09-06 14:12:26
1
DupyDago :
sasa hyo bi vers au frestyl
2026-09-13 02:06:58
0
Mzito :
Huyu siyo freestyler
2026-09-11 15:40:32
0
Gocher Mwashiga :
labda kwaya
2026-09-11 18:23:21
0
To see more videos from user @masterjimmy_tz, please go to the Tikwm
homepage.