@doctor.lucky14: Presha ya macho (eye pressure), hasa inapokuwa juu kwa muda mrefu, inaweza kuharibu neva ya kuona (optic nerve) inayounganisha jicho na ubongo. Mchakato huwa hivi: Presha ya macho kuongezeka → optic nerve kuanza kuharibika → uwanja wa kuona kupungua taratibu → uoni kuwa hafifu → ikichelewa kutibiwa, upofu wa kudumu unaweza kutokea. Tatizo kubwa ni kwamba mara nyingi glaucoma huanza bila maumivu au dalili wazi, hivyo mtu anaweza kuendelea na shughuli zake wakati neva ya kuona tayari inaharibika. #macho #afya #doctorprossy #matibabu