@jmtkaziiendeleeetz: MWAKA 2014 WALIKUWA MARAFIKI TU LEO PICHA HII IMEIBUA MAJINA MAKUBWA SERIKALINI Miaka 12 baadaye, picha moja ya harusi imegeuka kuwa simulizi ya nguvu kuhusu urafiki, uaminifu na safari ya maisha ya viongozi wa Tanzania. Mwezi Mei 2014, Mheshimiwa Antony Mtaka, ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, alifunga ndoa katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kigurunyembe, Morogoro. Wakati huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero. Mtaka anasema hakuwachagua Best Man na wasindikizaji wake kwa kuangalia vyeo, bali urafiki wa kweli. Katika picha hiyo, kutoka kushoto ni Sixtus Mapunda, alikuwa mtumishi wa CCM makao makuu Idara ya SUKI ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke; David Kihenzile ambaye alikuwa Afisa Mtendaji Kata ya Sinza Dsm sasa Naibu Waziri wa Uchukuzi; Mtaka mwenyewe; na Deo Ndejembi alikuwa anafanya kazi kampuni ya simu TIGO ambaye leo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Picha ilipigwa na Anthony Mavunde, ambaye wakati huo alikuwa wakili na siku hiyo alikuwa dereva wa maharusi,ambaye hivi sasa ni Waziri wa Madini. Mtaka anaeleza kuwa miaka imewapitisha kwenye nyakati za furaha, changamoto na majukumu mbalimbali, lakini urafiki ukaendelea kuwa daraja la ushauri na kutiana moyo. Kuhusu Makamu wa Rais Ndejembi, Mtaka anasema ni “mtu muungwana, mshirikishaji na mnyenyekevu”, anayesikiliza zaidi kuliko anavyoongea. Historia hii inakumbusha jambo moja: cheo kinaweza kubadilika, lakini urafiki wa kweli huendelea kuishi. #trendingsong #pppppppppppppppp #kenyantiktok🇰🇪 #tanzaniatiktok🇹🇿🇹🇿❣️🇰🇪🇰🇪♥️ #dodomatanzania🇹🇿
JMT kazi iendeleeetz🇹🇿
Region: TZ
Wednesday 02 September 2026 03:43:04 GMT
Music
Download
Comments
user9935005362045 :
Mh Mtaka utakuja kua Raisi siku moja wew ni kiongozi bora mnoo kuwahi kutoke NOTE IT
2026-09-02 11:31:33
2
asnathshigongo :
mzidishe upendo wenu tuu.
2026-09-02 09:33:27
1
mashaka j malewa :
nimebadilika maisha kupitia ww bro
2026-09-02 18:46:50
0
ZANZIBAR SHOP TEXTILES :
wa pili kutoka Kulia si ni KYLIAN MBAPE
2026-09-02 19:39:54
0
Pelagia Weiss :
mwaka 2030 muheshimiwa mtaka tafadhali chukua form ya kugombea urais.ingawaje haunijui utanijua mwaka huo.
2026-09-02 16:50:27
0
Sabu Yona :
katika viongozi apa tanzania ambaye nimewahi ongea naye ana kwa ana ni muheshimiwa mtaka ww ni hazina katika hili taifa mungu akuweke sana ww ni kiongozi bora sana
2026-09-02 20:19:43
0
user9935005362045 :
sio rahisi kila kitu nimunganiko wa matukio, niliwa kupiga picha na kiongozi na wenzangu wote wana nafasi serekalini ila mimi niliingilia tu kuomba kupiga picha ndo nipo nachezea Rumba aisee AMEEN
2026-09-02 11:30:05
0
mashaka j malewa :
aise mheshimiwa mtaka nakukubali sana ila inavutu vimenibadilisha maisha mm
2026-09-02 18:46:04
0
Jm :
mtaka my role model by DR JILALA (NJOMBE]
2026-09-02 16:34:43
0
Kemmy Rwechungula Francis :
kifupi wote ni mawaziri kasoro Mr Mtaka, ipo siku na yeye atateuliwa.
hongera kwao kwa kweli.
2026-09-02 10:27:26
1
To see more videos from user @jmtkaziiendeleeetz, please go to the Tikwm
homepage.