@katorotv: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Geita, Alexander Mnyeti kusimamia vyema shughuli za uchimbaji wa madini Mkoani humo, hususan katika Mji wa Katoro unaofahamika kwa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini. Akizungumza leo Septemba 2, 2026 katika Ikulu ya Tunguu, Zanzibar, Rais Samia amesema Mnyeti anapaswa kuhakikisha Wachimbaji na Wafanyabiashara wa madini wanaendelea kufanya shughuli zao kwa kufuata taratibu, kulipa kodi na kuchangia maendeleo ya Mkoa wa Geita.