@kusagatv: ASKOFU BAGONZA: VIONGOZI WASIUCHUKIE UKWELI BAADA YA KUPATA UONGOZI Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Askofu Dkt. Benson Kalikawe Bagonza, ametoa wito kwa viongozi na jamii kwa ujumla kutokuchukia ukweli, akisema tabia hiyo inaweza kubomoa mambo mengi mazuri ambayo jamii imeyajenga kwa gharama kubwa. Askofu Bagonza amesema kwa sasa kuna chuki kubwa dhidi ya ukweli katika jamii, huku watu wanaosema ukweli wakichukiwa na kubaki wapweke, licha ya ukweli kuwa ni miongoni mwa sifa muhimu zinazomfanya mtu astahili kuwa kiongozi. Amesema kinachotia hofu ni baadhi ya viongozi kuanza kuuchukia ukweli baada ya kupata nafasi za uongozi, wakati ukweli huo huo ndio uliowafanya waaminike na kupata uongozi. Kwa mujibu wa Askofu Bagonza, baadhi ya viongozi hujizunguka na wasaidizi wanaowaficha ukweli na kuwaambia mambo wanayotaka kuyasikia, hali inayoweza kuwafanya viongozi kushindwa kutambua hali halisi ya jamii wanayoiongoza. Amesema jamii inaweza kufanikiwa kufanya mambo mengi mazuri, lakini kuuchukia ukweli na kuwachukia watu wanaosema ukweli ni sawa na kubomoa yale yote yaliyokwisha jengwa kwa gharama kubwa. Askofu Bagonza amesisitiza umuhimu wa kuthamini watu wa kweli na kuupa nafasi ukweli, akieleza kuwa uongozi unaojengwa bila kusikiliza ukweli unaweza kuathiri maendeleo na kupoteza misingi iliyowekwa kwa ajili ya jamii.
MWANDISHI WA WANANCHI
Region: TZ
Wednesday 02 September 2026 21:13:57 GMT
Music
Download
Comments
Baby manka 5❤️💕 :
Baba askof Shikamooo me naomba mtaji
2026-09-03 03:02:46
0
Martin :
kabisa
2026-09-03 08:27:31
0
peoples favourite :
wakweli wanaumia sana
2026-09-03 07:56:29
0
🤑Amon_tz🤑 :
fact
2026-09-02 21:33:33
1
RN :
kabisaaaaaa
2026-09-03 06:02:42
0
RICHARD NGOWI :
Tanzania
2026-09-03 07:34:22
0
evanlee487 :
2026-09-03 07:31:51
0
Matoo :
r
2026-09-03 04:07:05
0
Tradermaryflorence :
kbs baba hasahas ccm n police 🙌🙌🙌 ila chawa wanapendwa
2026-09-02 21:25:37
0
mil :
Huyu apewe mufti. Aliyepo akalime kwao Lushoto
2026-09-02 22:49:16
0
To see more videos from user @kusagatv, please go to the Tikwm
homepage.