@iem_pius: Leo nakupa siri 6 nzito ambazo wafanyabiashara wengi wakubwa hawakwambii. Siri hizi zimenisaidia kupata wateja sahihi, kukuza biashara yangu na kuokoa muda. 1️⃣ BIASHARA YEYOTE SI NJIA YA MKATO Usianze biashara ukifikiri kila siku utapata faida. Kutakuwa na siku nzuri na siku ngumu. Changamoto sio ishara kwamba umefeli. Mara nyingi changamoto ndiyo inakufundisha namna ya kuwa mfanyabiashara bora zaidi. 2️⃣ MTAJI MKUBWA ZAIDI SI FEDHA, NI MAARIFA Unaweza kuwa na mtaji mkubwa, lakini kama hujui kuuza, kutafuta wateja, kutunza fedha, kujenga mfumo na kujifunza, mtaji unaweza kuisha. WEKEZA KWENYE KICHWA CHAKO KABLA HUJAWEKEZA KWENYE BIASHARA YAKO. 3️⃣ SIO KILA MTEJA NI WAKO Hili ni kosa ambalo wafanyabiashara wengi hufanya. Unajaribu kuuza kwa kila mtu mpaka unachoka. Ukijua vizuri nani unamtumikia, ana tatizo gani na kwa nini anahitaji bidhaa au huduma yako, unakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kupata wateja sahihi. 4️⃣ KILA MTU ALIANZA MAHALI FULANI Usijilinganishe na mtu ambaye amekuwa kwenye biashara kwa miaka 5 na wewe umeanza miezi 3 iliyopita. Mafanikio unayoyaona leo ni matokeo ya hatua nyingi ndogo ambazo huenda hukuziona. 5️⃣ MAFANIKIO HUONEKANA “OVERNIGHT” KWA WATU WASIOJUA SAFARI Watu wanaona siku umefanikiwa. Hawaoni siku ulizokataliwa, Hawaoni ulipoanguka, Hawaoni ulivyojifunza, Hawaoni miaka ya majaribio. Ndiyo maana usikubali mtu akufanye uamini kwamba mafanikio makubwa yanapatikana ndani ya siku chache. 6️⃣ NETWORK NA TEAMWORK NI MUHIMU SANA Kujenga biashara sio safari ya mtu mmoja. Watu sahihi wanaweza kukupa maarifa, connections, opportunities na support ambayo usingeipata ukiwa peke yako. Usiingie kwenye biashara ukiamini kwamba maombi pekee ndiyo yatakayokufanikisha. Muombe Mungu, ndiyo, Lakini pia tumia akili zako, jifunze, tafuta maarifa, tengeneza mikakati, jenga network, jifunze kuuza na chukua hatua. Na kama wewe ni mfanyabiashara, usikubali picha nzuri za watu mtandaoni zikufanye udhani kwamba wao hawapiti changamoto. Kila mafanikio yana story ambayo hujaiona. Kama Unataka Kuanza Biashara Kwa Muda Wa wako wa ziada nitumie Ujumbe Wenye Neno “BIASHARA”Kwenda WhatsApp 0756133313 #tiktok #viral #trending #trendingvideo #trendingreels
Pius Kichere🇹🇿
Region: TZ
Thursday 03 September 2026 11:54:56 GMT
Music
Download
Comments
ally sharifu :
ukitaka kujua msikilize I P M profet utajua hizo siri
2026-09-03 14:49:22
5
martin Davidy :
ukisema ukwel hautak fanikiwa
2026-09-03 13:42:41
3
Simba African King :
Ni kweli kabisa
2026-09-04 03:14:49
1
Joel borntaun :
kweli
2026-09-03 15:57:27
2
Simba African King :
Braza nakuunga mkono
2026-09-04 03:15:53
1
To see more videos from user @iem_pius, please go to the Tikwm
homepage.